Oscar Pistorius
Mwanariadha wa Afrika Kusini
asiye na miguu yote miwili Oscar Pistorius ameathirika vibaya kutokana
na ulemavu wake, daktari wa michezo ameiambia mahakama inayosikiliza
kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha huyo.
Wayne Derman ameiambia mahakama mjini Pretoria
kuwa bingwa huyo wa olimpiki ameathirika vibaya "kutokana na msongo wa
mawazo na hofu".Bwana Pistorius anasema alimuua kwa kumpiga risasi rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp baada ya kumdhania ni mwizi aliyeingia ndani ya nyumba yao mwaka jana.
Upande wa mashitaka unasema kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi Bi Steenkamp baada ya kuzozana.
Suala linaloangaliwa ni akili ya Pistorius wakati akifyatua risasi dhidi ya Reeva.
0 comments:
Post a Comment