SIMBA YATAKIWA IUNDE KAMATI YA MAADILI KABLA JUNI 30!
RAGE KUENDELEA KITINI!!
Uchaguzi Mkuu Simba ulipangwa kufanyika
Juni 29 na uamuzi huu wa TFF uliotangazwa Leo kwenye Mkutano wake na
Wanahabari unaitaka Simba kuunda Kamati ya Maadili ifikapo Juni 30 na
Kamati hiyo ndio itakayoshughulikia masuala yote ya Maadili kuelekea
kwenye Uchaguzi Mkuu.
Uamuzi huu wa TFF unaendelea kumweka
Madarakani Mheshimiwa Ismail Aden Rage hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika
baada ya Katiba yao kurekebishwa na kujumuisha Kamati ya Maadili.
Uchaguzi wa Simba umekumbwa na vuta
nikuvute Klabuni hasa baada ya Mgombea Michael Wambura kuenguliwa
kugombea Urais na Kamati ya Uchaguzi ya Simba na yeye kukata Rufaa TFF
ambako Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake
Wakili Julius Lugaziya, ilimpitisha na kuamua aruhusiwe kugombea.
Hivi karibuni, Yanga walipitisha
uundwaji wa Kamati ya Maadili ya Klabu yao ili kutii amri ya TFF kwenye
Mkutano Mkuu wao huko Bwalo la Polisi –Oysterbay, Jijini Dar es Salaam.
Lakini hatua hiyo ililazimu Mkutano huo
kumwongezea muda wa Mwaka mmoja Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji,
ili aweze kukamilisha masuala ya marekebisho ya Katiba yao na kujumuisha
Kamati ya Maadili na pia kuweza kuandaa Mkutano wa Uchaguzi baada ya
Katiba mpya kupitishwa na TFF
0 comments:
Post a Comment