JUMATATU
Usiku huko Arena Fonte Nova Jijini Salvador Nchini Brazil lile ‘KUNDI
la KIFO’, Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia, litaanza Mechi zake kwa
Germany kuivaa Portugal.
Baadae Usiku huo, huko Estadio das Dunas, Mjini Natal, Ghana itacheza na USA kwenye Mechi ya Pili ya Kundi hilo.
Kwa Wadau wengi Germany v Portugal ndio
mpambano wenyewe huku wengi wakitaka kumuona Mchezaji Bora Duniani,
Cristiano Ronaldo, akijaribu tena kuibeba Nchi yake kama alivyoifikisha
Fainali hizi kwa kuiteketeza ‘Mashine ya Kijerumani’.
Miezi 6 iliyopita Germany ilionekana
ndio tishio kubwa Duniani lakini baada ya hapo ikafifia baada ya
kukabiliwa na Majeruhi kwa Wachezaji kadhaa muhimu, utata wa Kocha
Joachim Löw katika kuteua Wachezaji na hata pia uchezaji hafifu kwenye
Mechi za Kirafiki.
Baada ya kuwa Majeruhi kwa kitambo,
Kambi ya Germany imethibitisha Kipa wao Manuel Neuer na Nahodha Philipp
Lahm wako fiti na wataanza Mechi hii.
Lakini Lahm huenda asichezeshwe Fulbeki
ya Kulia kama kawaida yake na badala yeke kucheza Kiungo ili kumpisha
Mchezaji mwenye nguvu, Jerome Boateng, kumkabili Ronaldo ambae Kocha wa
Portugal, Paulo Bento, humchezesha pembeni Kushoto.
Bila ya wasiwasi, Masentahafu wa Germany
watakuwa Per Mertesacker wa Arsenal na Mats Hummels wa Borussia
Dortmund na Fulbeki Kushoto atacheza Benedikt Höwedes au Erik Durm.
Kiungo wanatarajiwa kusimama Lahm,
Bastian Schweinsteiger na Sami Khedira lakini ikiwa watakosekana basi
Toni Kroos na Mesut Ozil wanaweza kuziba pengo huku mbele wakiwepo Lukas
Podolski na Mario Goetze.
Kwa upande wa Portugal, bila shaka, tegemezi kubwa ni Cristiano Ronaldo.
Kipa, bila mjadala, ataanza Eduardo na
Masentahafu ni Bruno Alves na Pepe huku Fabio Coentrao akicheza Fulbeki
ya Kushoto na Kulia ni Joao Pereira.
Kocha Paulo Bento, Siku zote hupenda
Kiungo ya Mtu 3 na hao ni Raul Meireles, Joao Moutinho na Miguel Veloso
ingawa William Carvalho yupo tayari kuchukua nafasi ya yeyote
atakaekosekana.
Fowadi ya Portugal itakuwa na Nani upande wa kulia, au Silvestre Varela, kati ni Hugo Almeida na Kushoto ni Ronaldo.
VIKOSI VINATARAJIWA:
PORTUGAL [Mfumo 4-3-3]:
-Eduardo
–Pereira, Alves, Pepe, Coentrao
–Veloso, Meireles, Moutinho
–Nani, Almeida, Ronaldo
GERMANY [Mfumo 4-2-3-1]:
-Neuer
–Boateng, Mertesacker, Hummels, Höwedes
–Lahm, Khedira
–Müller, Özil, Podolski
–Götze
Refa: Milorad Mazic [Serbia]
KOMBE LA DUNIA
Ratiba:
Saa za Kibongo
JUMATATU, JUNI 16, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Germany v Portugal |
G |
Arena Fonte Nova |
2200 |
Iran v Nigeria |
F |
Arena da Baixada |
0100 |
Ghana v United States |
G |
Estadio das Dunas |
0 comments:
Post a Comment