Leo Messi anatinga Estadio Maracana
Jijini Rio De Janeiro wakati Argentina itakapoanza kampeni zake kwa
kucheza na Bosnia-Herzegovina katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi F.
Baada ya kudorora kwa Lionel Messi Miaka
minne iliyopita kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini,
Mwaka huu tena mimacho iko kwake kuona nini atafanya.
Lakini Lejendari wa Argentina, Diego
Maradona, anamatumaini Staa huyo atawika hasa baada ya ‘kupumzika’ kwa
kukosa Mechi nyingi Msimu huu uliokwisha Juzi kutokana na kukabiliwa na
Majeruhi.
Maradona ameeleza: “Naona Messi atafanya
vizuri. Nadhani ilikuwa vyema kwake kupumzika baada ya kucheza Miaka
minne bila kukosa hata Mechi moja.”
Maradona aliongeza: “Ningependa kuongea
nae hivi sasa na kumwambia achukulie vitu kiulaini na asiwasikilize
Wajinga. Bahati mbaya wako wengi hao!”
Akiielezea Timu ya Argentina kwa ujumla,
Maradona ameonyesha wasiwasi wake kuhusu Difensi yao ambao Usiku huu
itapambana na Bosnia yenye Wachezaji wasio na mzaha kama vile Edin Dzeko
wa Manchester City.
Hata hivyo Safu ya Mashambulizi ya
Argentina inampa mchecheto hata Kocha wao Alejandro Sabella na asijue
acheze Fomesheni yake anayoipenda ya 5-3-2 au ya Mashambulizi ya 4-3-3.
Lakini, Wachambuzi wa Argentina,
waliofuatilia Mazoezi ya Timu hiyo Wiki hii wanahisi Sabella atampiga
Benchi Gonzalo Higuain na kuimarisha Safu ya ulinzi na hivyo kutumia
5-3-2 huku mbele wakiwa Aguero na Lavezzi na nyuma yao Messi.
Nae Kocha wa Bosnia, Safet Susic, amesema hawana mpangu kumuwekea Messi Mlinzi maalum.
Ameeleza: “Si vyema kwetu kupoteza
Mchezaji mmoja ili amlinde Messi. Hatujawahi kucheza Mechi tukiwa na
Mchezaji wetu kazi yake moja tu kumlinda Mtu mmoja na hili halitaanza
kwa Argentina!”
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa
Bosnia-Herzegovina kucheza Kombe la Dunia kwani ni Nchi changa iliyokuwa
huru Mwaka 1995 baada kusambaratika kwa Yugoslavia..
Pamoja na Timu hizi mbili, Timu nyingine Kundi F ni Iran na Nigeria ambazo zitakutana Kesho.
VIKOSI VINATARAJIWA:
ARGENTINA: Romero: Zabaleta, Garay, Fernandez, Rojo; Gago, Mascherano, Maria; Messi, Aguero, Lavezzi.
BOSNIA-HERZEGOVINA: Begovic: Mujdza, Bicakcic, Spahic, Kolasinac; Misimovic, Pjanic, Salihovic, Lulic; Ibisevic, Dzeko.
Refa: Joel AGUILAR [El Salvador]
KOMBE LA DUNIA
Ratiba:
**Saa za Bongo
JUMAPILI, JUNI 15, 2014 | |||
SAA | MECHI | KUNDI | UWANJA |
1900 | Switzerland v Ecuador | E | Nacional |
2200 | France v Honduras | E | Estadio Beira-Rio |
0100 | Argentina v Bosnia | F | Estadio do Maracanã |
JUMATATU, JUNI 16, 2014 | |||
SAA | MECHI | KUNDI | UWANJA |
1900 | Germany v Portugal | G | Arena Fonte Nova |
2200 | Iran v Nigeria | F | Arena da Baixada |
0100 | Ghana v United States | G | Estadio das Dunas |
0 comments:
Post a Comment