Sunday, 15 June 2014

KOMBE LA DUNIA: ECUADOR WALA KICHAPO CHA BAO 2-1 NA USWISI ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZINGINE



SWISS_v_ECUADORECUADOR, wakiongozwa na Staa wa Manchester United Antonio Valencia Usiku huu wamelimwaga baada kuongoza Bao 1-0 na kuiruhusu Uswisi kuwafunga 2-1 katika Mechi yao ya Kwanza ya Kundi E la Fainali za Kombe la Dunia kwenye Mechi iliyochezwa huko Estadio Nacional Mjini Brasilia.
Kitu cha kusikitisha mno kwa Ecuador ni kuwa kwenye Dakika ya 92, huku Bango likiwa tayari limeashiria Dakika 3 za Nyongeza, Antonio Valencia alichanja mbuga na kuingia ndani ya Boksi na kumpa Pasi murua Arroyo amalizie tu lakini Mchezaji huyo alifanya mbwembwe na Mpira kunaswa na Behrami na Uswisi kuanza shambulizi lao la nguvu ambalo walifunga Bao lao la ushindi.
Bao hilo lilifungwa na Haris Seferovic kwenye Dakika ya 92 na Sekunde 41.

MAGOLI
ECUADOR 1
-Enner Valencia Dakika ya 22
SWITZERLAND 2
-Admir Mehmedi Dakika ya 47
-Haris Seferovic 90 +2:41

Mechi zinazofuata kwa Ecuador ni dhidi ya Honduras Ijumaa Juni 20 wakati Uswisi itacheza na France Siku hiyo hiyo.
VIKOSI:
SWITZERLAND: Benaglio, Lichtsteiner, Rodriguez, Von Bergen, Djourou, Inler, Behrami, Shaqiri, Xhaka, Stocker, Drmic.
ECUADOR: Dominguez, Paredes, Ayovi, Guagua, Erazo, Antonio Valencia, Noboa, Gruezo, Montero, Caicedo, E. Valencia.
Refa: Ravshan IRMATOV [Uzbekistan]
KOMBE LA DUNIA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Switzerland 2 Ecuador 1
E
Nacional
2200
France v Honduras
E
Estadio Beira-Rio
0100
Argentina v Bosnia
F
Estadio do Maracanã
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Germany v Portugal
G
Arena Fonte Nova
2200
Iran v Nigeria
F
Arena da Baixada
0100
Ghana v United States
G
Estadio das Dunas
 

Hapo jana nayo Ivory Coast yawika Brazil

 
Ivory Coast ikishambulia lango la Japan
Miamba ya soka barani Afrika Ivory Coast imeimarisha matumaini ya bara hili baada ya kutoka nyuma na kuishinda Japan kwa mabao mawili kwa moja.
Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Gervinho huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda.
Ushindi huo wa Ivory Coast ni wa kwanza miongoni mwa timu za bara hili na unaiweka timu hiyo sawa kwa pointi na Colombia ambayo iliifunga Ugiriki mabao matatu bila jibu.
Ikiwa ni mara ya tatu kwa Ivory Coast kushiriki katika michuano ya Kombe la dunia,haijawahi kufuzu kupitia michuano ya kimakundi.
Hatahivyo chombo kilikuwa chaenda mrama baada ya kocha Sabri Lamouchi kuwashangaza wengi alipomuacha nje aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na kusababisha miamba hiyo kuwa chini kwa bao moja ilipofikia kipindi cha mapumziko.
Japan ambayo ndio mabingwa wa bara Asia walikuwa hatari katika ngome ya Ivory Coast kila walipopata mpira na walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 16 kutoka mshambuliaji wao Honda.
Mchezaji huyo wa kiungo cha kati anayeichezea kilabu ya A.C Milan alipata pasi murwa karibu na lango la upinzani kabla ya kupiga mkwaju mkali uliomuacha mlinda lango wa Ivory Coast kinywa wazi

Related Posts:

0 comments: