Holland watawavaa Mabingwa Watetezi wa
Dunia Spain Leo Ijumaa huko Salvador Nchini Brazil katika Mechi ya
Kwanza ya Kundi B ikiwa ni kama marudiano baada ya Nchi hizi kukutana
Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010 na Spain
kushinda 1-0.
Huko Afrika Kusini, Holland, chini ya
Kocha Bert van Marwijk, walifungwa 1-0 katika Dakika za mwisho za Mechi
hiyo iliyokwenda Dakika 120 huku Refa Howard Webb wa England akitoa Kadi
za Njano 14 na Nyekundu 1 ikiwa ni Rekodi kwa Fainali ya Kombe la
Dunia.
Safari hii, Holland wako chini ya Kocha
Louis van Gaal na Robin van Persie amesema wao ni Timu nzuri na wana
Wachezaji Vijana kupita huko Afrika Kusini na ambao wako tayari
kuikabili Spain.
Hata hivyo, Van Persie amekiri Spain pia
ni Timu nzuri yenye Wachezaji wazuri akiwataja Diego Costa na Mchezaji
mwenzake wa Manchester United, Kipa David de Gea.
Uso kwa Uso
-Mechi: 9
-Spain: Ushindi 4
-Netherlands: Ushindi 4
Sare: 1
VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Casillas, Ramos, Pique, Alba, Martinez, Fabregas, Alonso, Iniesta, Silva, Costa, Villa
Netherlands: Cillessen; Blind, Indi, de Vrij, Vlaar, Janamat ; de Jong, Sneijder, Guzman ; Robben, Van Persie
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
RATIBA:
JUMAA, JUNI 13, 2014 |
|||||||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
||||
1900 |
Mexico v Cameroon |
A |
Estadio das Dunas |
||||
2200 |
Spain v Netherlands |
B |
Arena Fonte Nova |
||||
0100 |
Chile v Australia |
B |
Arena Pantanal |
||||
JUMAMOSI, JUNI 14, 2014 |
|||||||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
REFA |
|||
1900 |
Colombia v Greece |
C |
Estadio Mineirão |
Mark Geiger [USA] |
|||
2200 |
Uruguay v Costa Rica |
D |
Estadio Castelão |
Felix Brych [Germany] |
|||
0100 |
England v Italy |
D |
Arena Amazonia |
Bjorn Kuipers [Holland] |
|||
0400 |
Ivory Coast v Japan |
C |
Arena Pernambuco |
Enrique Osses [Chile] |
|||
0 comments:
Post a Comment