Tuesday, 17 June 2014

KOMBE LA DUNIA: NIGERIA, IRAN NGOMA NGUMU!!

Iran na Nigeria zimetoka 0-0 hapo Jana huko Arena da Baixada Jijini Curitiba Nchini Brazil katika Mechi ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia na hii ndio Droo ya kwanza ya Mashindano haya tangu yaanze Juni 12.
Nigeria walitawala Mpira lakini walishindwa kuipenya Iran inayofundishwa na Kocha wa zamani wa Manchester United Carlos Queiroz.
Nafasi safi za Nigeria zilikuwa Kipindi cha Kwanza wakati Ogenyi Onazi alipopiga nje na Ahmed Musa kukosa kwa Frikiki.
Na nafasi nzuri ya Iran ilikuwa ile ya Reza Ghoochannejad ambayo iliokolewa na Kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.
Kwenye Mechi nyingine ya Kundi F iliyochezwa Juzi, Argentina iliifunga Bosnia Bao 2-1.
Mechi zinazofuata za Kundi F ni Jumamoso Jini 21 Argentina v Iran na Nigeria v Bosnia-Herzegovina.
VIKOSI:
IRAN: Haghighi; Montazeri, Hosseini, Sadeghi, Pooladi; Hajsafi, Nekounam, Teymourian, Dejagah; Ghoochannejhad, Heydari.
Akiba: Ahmadi, Shojaei, Haghighi, Reza Jahanbakhsh, Ansarifard, Haddadifa, Mahini, Alenemeh, Rahmani, Beikzadeh, Beitashour, Davari/
NIGERIA: Enyeama; Ambrose, Oboabona, Omerou, Oshaniwa; Mikel, Onazi, Azeez, Moses; Musa, Emenike.
Akiba: Yobo, Uzoenyi, Gabriel, Egwuekwe, Odemwingie, Odunlami, Ejide, Babatunde, Nwofor, Uchebo, Agbim, Ameobi
Refa: Carlos Vera (Ecuador)
KOMBE LA DUNIA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Germany 4 Portugal 0
G
Arena Fonte Nova
2200
Iran 0 Nigeria 0
F
Arena da Baixada
0100
Ghana 1 United States 2
G
Estadio das Dunas
JUMANNE, JUNI 17, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium v Algeria
H
Estadio Mineirão
2200
Brazil v Mexico
A
Estadio Castelão
0100
Russia v South Korea
H
Arena Pantanal
 

Related Posts:

0 comments: