Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza kwa Timu
zote mbili ambazo zipo Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia pamoja na
Ghana na USA ambao wanapambana baadae Usiku huu.
Muller alitangulia kufunga Bao lake la
kwanza Dakika ya 12 kwa Penati iliyotolewa baada ya Mario Gotze
kuangushwa na Joao Pereira.
Mats Hummels alifunga Bao la Pili Dakika
ya 32 na ndipo ikafuatia Kadi Nyekundu katika Dakika ya 37 kwa Pepe
ambae alivaana na Muller na Refa kuamua ni Frikiki na yeye kumzonga
Mjerumani huyo aliekuwa kakaa chini na kuinamisha kichwa chake kwake
kumgusa Mullar kitendo ambacho Refa Milorad Mazic wa Serbia alichukulia
kama fujo.
Kabla Haftaimu, Muller tena akapiga Bao na kuifanya Germany 3 Portugal 0.
Kipindi cha Pili, Thomas Muller akaongeza Bao lake la 3 Dakika ya 78 na Germany kushinda Bao 4-0.
Mechi inayofuata kwa Germany ni Jumamosi Juni 21 na Ghana na Portugal kucheza na USA Jumapili Juni 22.
VIKOSI:
GERMANY:
01 Neuer
20 Boateng
04 Höwedes
16 Lahm
17 Mertesacker
05 Hummels (Mustafi - 73')
06 Khedira
18 Kroos
13 Müller (Podolski - 82')
08 Özil (Schürrle - 63')
19 Götze
PORTUGAL:
12 Patricio
21 João Pereira
05 Fábio Coentrão (Almeida - 65')
04 Miguel Veloso (Ricardo Costa - 45')
03 Pepe (KADI NYEKUNDU – 37’)
02 Bruno Alves
08 João Moutinho
16 Meireles
09 Hugo Almeida (Éder - 28')
17 Nani
07 Ronaldo
Refa: Milorad Mazic [Serbia]
KOMBE LA DUNIA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
JUMATATU, JUNI 16, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Germany 4 Portugal 0 |
G |
Arena Fonte Nova |
2200 |
Iran v Nigeria |
F |
Arena da Baixada |
0100 |
Ghana v United States |
G |
Estadio das Dunas |
JUMANNE, JUNI 17, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Belgium v Algeria |
H |
Estadio Mineirão |
2200 |
Brazil v Mexico |
A |
Estadio Castelão |
0100 |
Russia v South Korea |
H |
Arena Pantanal |
0 comments:
Post a Comment