LEO JUMAMOSI, Juni 14, Saa 7 Usiku, Arena Amazônia, Manaus, Brazil
KUNDI D la Fainali za Kombe la Dunia
huko Brazil Usiku huu zinaanza Mechi zao za kwanza kwa Uruguay kuivaa
Costa Rica huko Estadio Castelão Jijini Fortaleza na kufuatia ule
mtanange unaongojewa kwa hamu, England v Italy.
PATA TAARIFA ZA WACHEZAJI/TATHMINI/REKODI/VIKOSI:
Hali za Wachezaji
Italy huenda wakalazimika kutumia
Masentahafu wa 3 nyuma badala ya kusimamisha Difensi ya Mtu 4 baada ya
Fulbeki wao Mattia De Sciglio kuumia Pajani.
Lakini habari njema kwa Italy ni zile za Mario Balotelli na Marco Verratti kupata afueni matatizo yao kiafya.
Tathmini
Kila Timu inatinga ndani ya Arena
Amazônia Jijini Manaus ikihofia athari za Joto na hivyo watacheza Soka
la tahadhari la kumiliki Mpira ili wasiupoteze ovyo na kupoteza nguvu
ovyo kwa kuukimbiza kutaka kuumiliki tena.
Kama ilivyokuwa kwenye EURO 2012, Mpishi
mkuu wa Italy ni Mkongwe Andrea Pirlo, ambae sasa ana Miaka 35, na
ambae huko Kiev Miaka minne iliyopita alitoa Pasi nyingi kupita Wacheza
wote wa Kiungo wa England na kuzunguka umbali mrefu kupita Mchezaji
yeyote wa England kwenye Mechi hiyo ya EURO 2012.
Lakini England ya hivi sasa, chini ya
Meneja Roy Hodgson, ni ya Chipukizi wengi, kina Daniel Sturridge, Raheem
Sterling na Ross Barkley, wakiongezwa nguvu na Wakongwe Steve Gerrard,
Frank Lampard na Wayne Rooney.
Uso kwa Uso
-Jumla Mechi 24
-England: Ushindi Mechi 8 Magoli: 30
-Sare: 7
-Italy: Ushindi 9 Magoli: 27
Dondoo muhimu
-Mara pekee kwa England na Italy
kukutana kwenye Kombe la Dunia ni kwenye Mechi ya kuwania Mshindi wa
Tatu Mwaka 1990 ambayo Italy walishinda 2-1.
-England wameshinda Mechu 2 tu kati ya 11 walizocheza mwisho dhidi ya Italy wakifungwa 6.
-Mara ya mwisho kukutana ilikuwa huko Switzerland Mwezi Agosti Mwaka 2012 na England kushinda 2-1.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA:
England: Hart, Johnson, Jagielka, Cahill, Baines, Gerrard, Henderson, Lallana, Sterling, Rooney, Sturridge
Italy: Buffon, Abate, De Sciglio, Bonucci, Chiellini, De Rossi, Pirlo, Verratti, Candreva, Marchisio, Balotelli
REFA: Bjorn Kuipers [Holland]
JUMAMOSI, JUNI 14, 2014 |
||||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
REFA |
1900 |
Colombia v Greece |
C |
Estadio Mineirão |
Mark Geiger [USA] |
2200 |
Uruguay v Costa Rica |
D |
Estadio Castelão |
Felix Brych [Germany] |
0100 |
England v Italy |
D |
Arena Amazonia |
Bjorn Kuipers [Holland] |
0400 |
Ivory Coast v Japan |
C |
Arena Pernambuco |
Enrique Osses [Chile] |
0 comments:
Post a Comment