Saturday, 14 June 2014

MAXIMO KUAMUA WANAOINGIA, WANAOTOKA YANGA



Kocha mtarajiwa wa Yanga, Marcio Maximo ndiye atakuwa anapendekeza wachezaji anawaowataka kwa ajili ya kuboresha kikosi chake.


Taarifa zinaeleza, baada ya Maximo kuomba apewe nguvu ya mwisho kwenye usajili, Yanga imekubali kumkabidhi.

Habari za uhakika kutoka kwa upande wa wakala anayeshughulikia ujio wa Maximo zinaeleza sasa atakuwa akipendekeza na kusajili wachezaji anaoamini watakisaidia kikosi chake.
“Sasa makubaliano ni asilimia zaidi ya 95, wakati wowote anakuja na tayari kocha ameomba kupewa rungu la usajili na imekubalika,” alisema.
Maximo ndiye kocha mtarajiwa kuziba pengo la Hans van der Pluijm, raia wa Uholanzi ambaye ameondika baada ya kupata dau la juu.
Lakini imekuwa ikielezwa wachezaji wa Yanga wamekuwa na hofu kuhusiana na ujio wake na hasa Juma Kaseja na Athumani Iddi Chuji ambao wamekuwa hawaelewani.
Lakini uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa bado uko kwenye mazungumzo na kocha huyo na masuala mengine yote yanawezekana.

Related Posts:

0 comments: