TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI WILAYANI MOMBA MAJIRA YA SAA 10:30 NA MWINGINE SAA 10:40 ASUBUHI.
MTUHUMIWA
WA KWANZA TATU MWAMPASHI (25) ALIKAMATWA KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA
YA KIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA AKIWA NA
NOTI BANDIA 31 KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS
155,000/=ZOTE ZIKIWA NA NAMBA AA0845926.
AIDHA
MTUHUMIWA WA PILI ANGOMWILE KAPUNGU (26) ALIKAMATWA KATIKA KITONGOJI
CHA SIKANYIKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA
AKIWA NA DOLA BANDIA 2 @ THAMANI YA USD 100 ZIKIWA NA NAMBA
BL-72830434-A NA FT-85311229-H.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYWA.
KATIKA MSAKO MWINGINE:
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAILOS KAYANGE (45) MKAZI WA MBOZI
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA VIPODOZI
MBALIMBALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI KATIKA
MTAA WA MWAKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA
MBEYA. VIPODOZI HIVYO NI PAMOJA NA BELTASON DAZANI 10, EPIDERM DAZANI 4
NA CARLORIGHT KATONI 01 ZOTE ZIKIWA ZIMETOKA NCHINI ZAMBIA.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA
UINGIZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU
WANAOJIHUSISHA NA MTANDAO WA UTENGENEZAJI NOTI BANDIA HAMA UINGIZAJI NA
UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI ILI WAKAMATWE NA HATUA
ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment