Rais
Kenyatta akiwa na timu ya taifa Harambee Stars katika Ikulu mjini Nairobi
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe
Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia
Hafla
ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais
Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya
usafiri kwenda Brazil.
Mmoja
wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao
imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano,
malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama.
Kitendo
cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya
taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika
duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye
mwakani.
Hatua
ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya
taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji
hatua yake itasaidia nini?
Soka
ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji
kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya.
Kenyatta
na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa
kima cha dola elfu arobaini. Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake
hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini
Kenya.
Pia
ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe
la Cecafa.
Kenyatta
mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema
wa Kenya nchini Brazil.
Ufadhili
huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara kocha wa
timu hiyo kwa miaka miotano ijayo.
Kenya
haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa
Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya
taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa
kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.
CHANZO: BBCSWAHILI
0 comments:
Post a Comment