Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi Mh. Paul Lwanji wakinyanyua bati juu kuwapatia mafundi wanaojenga madarasa katika shule ya sekondari ya Mgandu wakishiriki ujenzi wa shule hiyo wakati Katibu mkuu huyo alipokagua ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ikiwa ni ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Singida, Tabora na Manyara ambapo leo amewasili katika mkoa wa Singida baada ya kumaliza ziara yake katika mkoa wa Tabora akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifukia mti mara baada ya kupanda mti katika shule ya sekondari ya Mgandu leo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akipanda mti katika shule ya sekondari ya Mgandu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua bwawa la umwagiliani katika kijiji cha Igala Itigi mkoani9 Singida
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Manyoni Bw. Deus Magoma wakati akielezea kuhusu mradi wa bwawa la la kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hicho.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria katika mkutano huo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutanohuo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
0 comments:
Post a Comment