Algeria,
Cameroon, Ghana na Nigeria zimetinga katika kushiriki fainali hizo ambazo
zinatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu sio pekee kwa timu zilizopangwa
kwenye makundi lakini pia kwa timu zinazotoka bara moja.
Ukilitazama
bara la Ulaya utakutana na ushindani usio kifani Ujerumani ikitaka kuweka
rekodi safi katika fainali hizo, hali kadhalika kwa Hispania dhidi ya Uholanzi.
Haitoshi
Italia itataka kuwapiku Ufaransa hali kadhalika Ureno nayo ikiwania nafasi
muhimu katika fainali hizo dhidi ya Uingereza pia Bosnia-Herzegovina.
Bara
la Amerika ya Kusini nalo pia linataka kulibakisha Kombe hilo barani humo, kukitarajiwa
kuwa na ushindani wa kukata na wembe, Argentina kuonyesha ubabe kwa Brazil,
Uruguay dhidi ya Chile.
Hivyo
barani Afrika hakuna asiwajua Tembo wa Afrika, jina lao zuri linaongeza ladha
kutokana na wazungu wengi kumfahamu Tembo kwa kutalii nchi za Afrika
wanakopatikana kwa wingi.
Ivory
Coast ambayo kwenye viwango vya soka imeshangaza nchi nyingi hata za barani
Ulaya kutokana na usakataji kabumbu wenye ladha ipo katika nafasi 25 za juu
kila mwezi inapotangazwa, kwa bara la Afrika imeshika nafasi ya kwanza kwa muda
mrefu sasa.
Akademi
ya ASEC Mimosas imetoa wakali Emmanuel Ebou, Didier Zokora, Salmon Kalou, Kolo
Toure na mdogo wake Yaya Toure isipokuwa Didier Drogba ambaye anawika bila
kutoka katika akademi hiyo maarufu.
Ivory
Coast inaandika historia nyingine katika Kombe la Dunia ikizama kwa mara ya
tatu, mwaka 2006, 2010 na 2014.
Je,
Tembo hao wa Afrika wa sasa, wataweza kuweka rekodi tamu na yenye kuvutia
kuzidi vikosi 4 bora ambavyo nimevianisha kutoka bara la Afrika vilivyowahi
kufanya mambo makubwa katika ulimwengu wa soka (African Golden Generations)?
KUNDI
C BRAZIL 2014
Katika
Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil makundi 8 yatachuana kusonga mbele katika
hatua ya 16, robo (8) , nusu (4) na fainali (2) ili kulinyakua Kombe hilo
ambalo linachezwa kwa mara ya 20 sasa.
Kundi
C linaundwa na Colombia, Ugiriki, Ivory Coast na Japan.
Colombia
inanolewa na Kocha Jose Pekerman, ambapo rekodi yake nzuri katika Kombe la
Dunia ni pale ilipofika hatua ya 16 katika Fainali za Kombe la Dunia 1990.
Mwaka
huu linamtegemea aliyezaliwa mfungaji Radamel Falcao ambaye atakuwa bega kwa
bega na mchezaji mwenzake wanayesakata kabumbu pamoja katika klabu ya AS
Monaco, Javier Rodriguez.
Ugiriki
inafundishwa na Fernando Santos, ikiwa na rekodi bora kufika hatua ya makundi
1994 na 2010.
Nchini
Brazil, Ugiriki macho na masikio yatakuwa kwa wazoefu wao Georgios Samaras
anayechezea klabu ya Celtic akiwa na mkongwe Dimitris Salpingidis katika safu
ya ushambuliaji ambao walitoa msaada mkubwa katika mechi za kufuzu.
Japan
ipo katika kundi hili chini ya uangalizi wa Kocha Alberto Zaccheroni, ikiwa na rekodi
ya kufika hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2002 na 2010.
Samurai
watakuwa wakitegemea umahiri wa nyota asiyechuja Keisuke Honda huku
Shinji Kagawa naye akitarajiwa kutoa msaada wa karibu kuhakikisha wanafikia
malengo, licha ya maneno mengi wakati wakiwa kwenye harakati za kufuzu.
Ivory
Coast inanolewa na Sabri Lamouchi ambaye alipokea kazi kutoka kwa Valid
Halidhozic anayeinoa Algeria. Tembo hao rekodi yao bora ni ile walipofika hatua
ya makundi katika fainali za Kombe la Dunia 2006 na 2010.
Safari
hii, Yaya Toure mchezaji bora barani Afrika 2013 na Kiungo mahiri Ligi Kuu
England msimu 2013/2014 ndiye anayekodolewa macho kutokana na aina yake ya
usakataji soka ulio makini.
Hata
hivyo hatakuwa peke yake atakuwa na watalaamu wengine ambao wameisaidia sana
timu hiyo katika michuano mbalimbali ya kimataifa Didier Drogba, Salmon Kalou
na Wilfred Bony.
4
AFRICAN GOLDEN GENERATIONS
Ivory
Coast inaingia katika wakati mgumu wa kuhakikisha ubora wao kwa vikosi
vifuatavyo vilivyowahi kufanya makubwa barani Afrika kwa takribani miongo
miwili.
- MISRI 2006-2010
Mpaka
sasa hakuna taifa lolote barani Afrika lililochukua Kombe la Mataifa ya Afrika
mara tatu (hat trick) mfululizo kati ya mwaka 2006 hadi 2010 isipokuwa ni
Misri.
Misri
ilifanya hivyo mwaka 2006, 2008 na 2010; hata hivyo kulingana na ushindani
mkubwa katika soka kwa sasa inaonyesha wazi kuwa hakuna taifa litakalofanya
hivyo katika miaka ya karibuni.
Wachezaji
wa kizazi hicho; Wael Gomaa na Essam El-Haddary walikuwepo wakati Mafarao
wakifanya kazi ya ziada, Ahmed Hassan, Hossam Hassan, Mohamed Aboutrika, Emad
Moteab, Amr Zaki, Gedo na Mido walitoa mchango mkubwa.
Wachezaji
hao wakati wakifanya hayo walio wengi walitoka katika klabu ya Al Ahly.
Licha
ya kuonyesha rekodi safi Misri ilishindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014
kutokana na mapinduzi ya kisiasa nchini humo, kabla ya hapo walikosa WOZA 2010
na kuwapa nafasi Cote d’Voire na Cameroon kutinga katika fainali hizo.
- NIGERIA 1994-1998
Katikati
ya miaka ya 1990; Nigeria ilikuwa inatisha katika soka barani Afrika ambapo
haikuchukua muda mwaka 1994 waliandika historia ya kutinga Kombe la Dunia
nchini Marekani.
Hata
hivyo Nigeria ambao walijikuta katika kikwazo kikubwa wakipangiwa na Argentina
walishindwa kufurukuta na kujikuta wakiishia hatua ya 16 bora.
Mwaka
1996 walifanya marekebisho makubwa na wakatwaa Medali ya dhahabu katika
michuano ya Olimpiki ya Atlanta.
Kutwaa
medali kwa Super Eagles kuliwatia wehu, ndipo wakatinga katika fainali za Kombe
la Dunia 1998 nchini Ufaransa na kwa kuonyesha wako vizuri, waliwazabua
Hispania (La Fuja Roja) katika mechi ya ufunguzi.
Utawakumbuka
wachezaji walioiwakilisha vizuri Nigeria miaka hiyo, Sunday Oliseh, Taribo
West, Finidi George, Jay Jay Okocha, Nwako Kanu na wengineo.
Ikilinganishwa,
Ivory Coast ya sasa ipo tofauti kabisa na Super Eagles ya wakati huo; kutokana
na wachezaji wake wengi kutokuwa na majina makubwa katika vilabu walivyokuwa
wakichezea.
- CAMEROON 2000-2003
Simba
wasioshindika “Indomitable Lions” walikuwa imara sana miaka ya 1980 hadi 1990
wakichukua mataji mawili ya AFCON na kuishia hatua ya robo fainali nchini
Italia.
Miaka
10 baadaye, kilizaliwa kizazi ambacho ni Kizazi cha Dhahabu, mwanzoni mwa karne
ya 21, Cameroon ilikuwa haikamatiki (unstoppable), wakitwaa AFCON 2000, miezi
michache baadaye walitwaa Medali ya Dhahabu Olimpiki nchini Australia.
Mwaka
2002, “Indomitable Lions” waliweka rekodi ya kwanza kuitungua Senegali kwa
penati mjini Bamako, nchini Mali tangu walipofanya hivyo 1965.
Hata
hivyo, mwaka 2003 walikumbwa na simanzi ya kuondokewa na nyota wao
waliyetengeneza kizazi cha dhahabu, Injini ya Cameroon Mac-Vivien Foe
alipoanguka katika Uwanja wa Stade Gerland na kufa papo hapo.
Pierre
Wome atakumbukwa sana akiikosesha bahati Cameroon kufuzu Kombe la Dunia 2006
wakati huo wakitokea kwenye machungu ya kuishia hatua ya robo fainali AFCON.
- GHANA 2009
Wakitokea
katika U-20 (Black Satellites), waliweka historia kwa bara la Afrika kwa kizazi
cha dhahabu, wakitwaa Kombe la Dunia U-20 nchini Misri.
Kocha
Milovan Rajevac aliwaona nyota Daniel Adjei, Samuel Inkoom, Jonathan, David
Addy, Emmanuel Agyemang-Badu, Andrew Ayew, Daniel Opare na Mohammed Rabiu na
kuwaingiza katika kikosi cha Black Stars.
Kikosi
hicho ndicho kilisababisha Ghana ikang’ara katika fainali za Kombe la Dunia
2010 nchini Afrika Kusini wakiishia robo fainali, wakikosa mkwaju wa penati
dhidi ya Uruguay ambao Luis Suarez aliokoa kwa mikono na kuwanyima kutinga
hatua ya nusu fainali.
Yaya Toure(31)
anaichezea Klabu ya Manchester City ambayo imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa
2013/2014 ikiwa ni taji la pili ndani ya miaka mitatu huku nyota huyo akitupia
mabao 20 katika Ligi Kuu nchini England.
Yaya
ameichezea Ivory Coast mechi 86 tangu mwaka 2004 na akifumania nyavu mara 16
Salmon
Kalou(28), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea sasa yupo Lille LOSC
amechezea Ivory Coast mechi 64 akitupia mabao 23.
Nyota
wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba (36), akiicheza na Galatasaray ya nchini
Uturuki ambapo vilabu vingine vipo mbioni kutaka saini ya yake baada ya Kombe
la Dunia ameichezea Ivory Coast mechi 99 akizifumania nyavu mara 63.
Mchezaji
wa siku nyingi wa Tembo wa Afrika, Didier Zokora (33) aliyeichezea Ivory Coast
na kuvunja rekodi ya kucheza mechi 118 na kutupia bao moja akisaidiwa na
Gervinho (AS Roma), Cheki Tiote (Newcastle), Wilfred Bony (Swansea) na wengineo
wataweza kuvipita vikosi hivyo vya dhahabu nilivyokuanishia hapo?
0 comments:
Post a Comment