HOME »
» LIGI KUU VPL KUANZA AGOSTI 24 TIMU 16 KUGOMBEA MWALI
RATIBA
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka Julai 24, mwaka huu na
michuano hiyo ya kusaka bingwa wa nchi itaanza mwezi mmoja baadaye,
Agosti 24 mwaka huu.
Taarifa
ya TFF leo, imesema kwamba usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza
msimu huu (2014/2015) wa ligi hiyo unaanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka
huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa
mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
 |
Mabingwa; Azam FC wataanza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Agosti 24, mwaka huu |
Kipindi
cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi
Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya
Agosti 4 na 11 mwaka huu.
Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.
Usajili
hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na
kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti
30 hadi Septemba 4 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni
Septemba 5 na 6 mwaka huu.
Kwa
upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka
huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka
huu).
Tayari
TFF imesema timu za Ligi Kuu msimu ujao zitaongezeka kutoka 14 za sasa
hadi 16, ingawa haijaweka wazi kama juu ya timu zitakazoongezeka kama
zitatoka katika zilizoshuka au zilizokosa nafasi ya kupanda katika mfumo
wa zamani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment