

Juhudi za kuanza kumsaka nyoka huyo zilianza siku chache baada ya
mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kutoa taarifa ya tahadhari
kwa wakazi juu ya uwepo wa nyoka huyo mkubwa katika eneo hilo na
kuwataka wakazi kuwa makini wanapopita katika njia za mkato zilizopo
kwenye maeneo anayotajwa kuonekana.
Wataalamu ambao ni waganga wa jadi wakishirikiana na
maafisa maliasili kutoka halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamefanikiwa kumnasa chatu
mdogo anayesadikiwa kuwa ni mtoto wa chatu ambaye amekuwa akionekana.
Wataalamu hao wakiongozwa na Mazoea Hamisi(30)
mkazi wa Chalinze mkoani Pwani wameweza kumnasa chatu mdogo
waliyemkuta pembezoni mwa Mto Meta jirani na hoteli ya Rift Valley.
Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini
kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo
alipofanikiwa kumkamata.
Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi
wa Chunya mkoani hapa, Chatu aliyekamatwa ni mdogo na juhudi za
kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo.
Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili
kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na
maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.
0 comments:
Post a Comment