KLABU
ya Free State Stars ya hapa imesema imekuwa ikimtaka sana mshambuliaji
wa Azam FC, John Raphael Bocco, lakini wanasikia hawawezi kumpata kwa
sababu mchezaji huyo ni kipenzi cha mmoja Wakurugenzi wa timu yake
Tanzania, Yussuf Bakhresa.
Meneja
Mkuu wa Free State, Rantsi Mokoena ambaye ni mtoto wa mmiliki wa timu,
Mike Makoena amesema kwamba wamejaribu mara kadhaa kutaka kumhamishia
Bocco Afrika Kusini, lakini inashindikana.
|
Yussuf Bakhresa analalamikiwa na Free State Stars kuwabania John Bocco |
“Bocco
ni mshambuliaji wa kiwango cha kidunia, Azam inakali mafanikio yake.
Kama anakuja hapa, akicheza kidogo tu mtamsikia yuko Ulaya. Ila tumekata
tamaa, tunasikia yule ni kipenzi cha mtoto wa mwenye timu (Yussuf),
anamlea vizuri naye ameridhika na maisha ya pale,”amesema Rantsi.
Kwa
upande wake, mtoto mwingine wa mwenye timu hiyo, Kootso Mokoena ambaye
ni Meneja wa timu amesema Tanzania ina wachezaji wazuri ambao amekuwa
akiwaona mara kadhaa.
“Nimekuwa
nikiwaona wachezaji wa Tanzania mara kadhaa, wakati fulani nilikuja Dar
es Salaam mkiwa mnacheza na Msumbiji mkafungwa 1-0, kuna mchezaji
nilimpenda pia, lakini nilipotaka kumchukua ikaibuka mizengwe,
nikaacha,”.
|
John Bocco anatakiwa sana Free State ya Afrika Kusini |
“Ngassa
(Mrisho) nilimuona Uganda mwaka juzi (kwenye Kombe la Challenge).
Nilimpenda tangu hapo, wakati wote nimekuwa nikimfuatilia bila
mafanikio, na sasa tunajaribu kwa mara ya mwisho,”amesema Kootsi.
Free
State Stars leo itatuma ofa ya nyongeza kidogo katika kujaribu kumnunua
Ngassa, baada ya klabu yake, Yanga SC kukataa ofa ya awali ya dola za
Kimarekani 80,000 zaidi ya Sh. Milioni 130, ikitaka dola 150,000 zaidi
ya Sh. Milioni 240.
Ngassa
tayari yuko hapa Bethlehem akifanya mazoezi na timu hiyo ya Ligi Kuu ya
Afrika Kusini, iliyomuajiri kocha wa zamani wa Yanga SC, Mbelgiji, Tom
Saintfiet na mwenyewe ameonyesha dhamira ya kubaki.
Mshambuliaji
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu aliwahi kuchezea
Free State mwaka 1997 wakati bado inaitwa Qwa Qwa Stars kabla ya
kununuliwa na familia ya Makoena mwaka 2003.
Wachezaji
kadhaa wakubwa wamepitia katika klabu hiyo akiwemo Bunene Ngaduane wa
DRC, Jonathan Mensah wa Ghana, Kennedy Mweene wa Zambia, John Tlale na
Siphiwe Tshabalala wote wa Afrika Kusini na ambao pia wapo Bafana
Bafana.
Na Mahmoud Zubeiry, BETHLEHEM
0 comments:
Post a Comment