Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa wakati akisoma taarifa wakati
akifungua mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa
unaohusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza
na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration
uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya waandishi wa habari
waliohudhuria mkutano huo wa NEC kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya
Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu
wa mkoa wa Iringa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkoa wa Iringa.
Baadhi ya waandishi wa habari
waliohudhuria mkutano huo wa NEC kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya
Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu
wa mkoa wa Iringa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkoa wa Iringa.
…………………………………………………………………….
TUME ya Taifa ya Uchaguzi
imetoa elimu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa kuhusu kusambaza
elimu juu ya mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
kwa wananchi juu ya mfumo mpya utakaotumika kuandikisha wapiga kura wa
mkoani hapa wa teknelojia ya kibailojia(BVR).
Tume inatarajia kufanya uboreshaji
wa daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni
kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric Vote Regstration (BVR).
Hayo yamebainishwa juzi mjini hapa
na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa wakati
akifungua mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa
unaohusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza
na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration
uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.
Jaji Mkwawa alisema lengo ni
kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura waliofika umri
wa miaka 18 na hawapo katika daftari la kudumu la kupiga kura,waliohama
makazi yao ya awali walikojiandikisha na wanajitokeza kwa wingi katika
vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema mfumo huo mpya ni wa
kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu
na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi na kutumia
kitambulisho kipya cha kupiga kura.
“Mfumo huu hutumika katika
kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za
binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura
watachukuliwa alama za vidole vyote kumi vya mikono, picha na saini
ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya
wapiga kura” Alisema Jaji Mkwawa
Jaji Mkwawa alisema kupiga kura
kwa Watanzania walio wengi sio lazima hivyo hawaoni thamani ya kupiga
kura, hivyo Vyombo vya Habari vinawajibu mkubwa wa kuelimisha umma juu
ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na
ni tofauti na nchi ya Shelisheli ambayo kujiandikisha na kupiga kura ni
lazima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Ruth Mashama akiwasilisha mada inayohusu maandalizi ya uboreshaji wa
Daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric
Vote Registration (BVR) ameeleza kuwa Tume inatarajia kuboresha Daftari
la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza hivi karibuni na maandalizi
yake tayari yamekamilika kwa sehemu kubwa na baadhi ya vifaa vimeanza
kuwasili nchini Tanzania.
Alisema matumizi ya mfumo mpya
utatumika katika zoezi la uandikishaji pekee tofauti na nchi nyingine
zilizotumia mfumo hadi katika kupiga kura na kugundua mafanikio
yaliambatana na changamaoto mbalimbali za kiteknolojia na kimfumo.
Mashama alizitaja baadhi ya nchi
za Kiafrika zilizokwisha tumia mfumo wa BVR kuwa ni Nigeria 2007,Ghana
2009,Liberia2005,Guinea 2005,Mali 2005, Uganda 2008,Kenya 2013,Zambia
2008, Afrika Kusini na Zanzibar 2009.
0 comments:
Post a Comment