GWIJI
wa Manchester United, Paul Scholes anaamini kwamba mshambuliaji wa
Liverpool, Luis Suarez anafanya makosa kutaka kusaini Barcelona.
Mshambuliaji
huyo mtata wa Uruguay anajiandaa kuhamia klabu hiyo ya Katalunya, baada
ya Liverpool kuingia majadiliano na viongozi wa Barcelona wiki hii,
kufuatia Suarez kufungiwa miezi mine baada ya kumng'ata beki wa Italia,
Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia.

Anakwenda kujimaliza? Paul Scholes anaamini kuliko kwenda Barcelona, Luis Suarez bora angeenda Real Madrid
Scholes hafikiri kwamba Suarez atacheza vizuri pamoja na mkali wa mabao wa Barcelona, Lionel Messi
Scholes,
pia amehoji kama Suarez ataendana Muargentina Lionel Messi katika
kikosi cha Barca na kisha amependekeza mshambuliaji huyo ni bora ahamie
Real Madrid.
"Ikiwa
Luis Suarez atasaini Barcelona kutoka Liverpool, je Lionel Messi
‘atamkubali yeye? Suarez ni mshambuliaji wa kati na hatataka kucheza
pembeni. Sioni namna gani Suarez na Messi watacheza pamoja,".
"Inasemekana
kwangu, ikiwa Messi atakupenda, utacheza. Asipokupenda huwezi,
unapoteza muda wako. Na, kwa kweli, nafikiri Suarez
anafanya makosa makubwa sana kwenda Barcelona – ni bora angehamia Real
Madrid,".
0 comments:
Post a Comment