MSHAMBULIAJI majeruhi, Neymar Jr atahudhuria mechi ya
mshindi wa tatu siku ya jumamosi kati ya nchi yake ya Brazil dhidi ya Uholanzi.
Brazil waliomkosa Neymar katika mechi ya nusu fainali dhidi
ya Ujerumani na kulala kwa mabao 7-1 watachuana na kikosi cha Louis van Gaal
ambao kilitolewa jana kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Argentina.
Neymar aliyeibeba Brazil mechi za nyuma alikosekana na
kusababisha nchi yake ifanyiwe kitendo cha `Ukatili` na Wajerumani.
Nyota huyo wa Barcelona alivunjika mfupa wa uti wa mgongo
wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Colombia nah ii ilitokana na kugongwa
kwa goti mgongoni na Juan Zuniga.
“Neymar atakuja hapa (kwenye kikosi cha Brazil). Lengo ni kuwasapoti
wachezaji wenzake kwenye mechi ya jumamosi”. Msemaji wa Shirikisho la Brazil,
Rodrigo Paiva amethibitisha alipozungumza na R7.com.
Paiva alitangaza taarifa hizo akiwa makao makuu ya fainali za kombe la
dunia, mjini Teresopolis, karibu na Rio de Janeiro.
Hata hivyo, wiki hii madaktari wa klabu ya Barcelona wameripotiwa
kumtembelea mshambuliaji huyo wa Barca akiwa nyumbani kwao.
Taarifa kutoka katika mtandao wa klabu ya Barcelona
ilisomeka: “Wiki hii Madaktari wa FC Barcelona walimtembelea Neymar Jr akiwa
nyumbani kwao nchini Brazil”.
“Viongozi wa CBF na madaktari wa Barca wapo katika
makubaliano kujua aina ya matibabu atakayopata ili kuimarika kiafya”.
Kukosekana kwa Neymar na beki aliyekuwa na adhabu, nahodha Thiago Silva kulichangia kwa kiasi kikubwa kufungwa mabao mengi na Ujerumani ambao watavaana na Argentina siku ya jumapili kwenye mchezo wa fainali wa kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment