Mchezaji Neymar baada ya kupata jeraha
Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .
Anatolea nje: Neymar akiwa amebebwa kwenye machela kutolewa née kabla ya kukimbizwa hospitali baada ya mechi
Rafu iliyomuumiza; Hakuwa na mpira wakati anapigwa kwa goti mgongoni na Camilo Zuniga
Akaenda chini kama mzaha
Akashika eneo la mgongoni alilopigwa
Beki Marcelo anamuombea msaada baada ya kugundua ameumia kweli
Anapatiwa huduma ya kwanza uwanjani
Nyota
wa Colombia, James Rodriguez anamkaribia Neymar kumtaka ainuke kutoka
nje mchezo uendelee kuokoa muda wajaribu kusawazisha bao, wakati huo
tayari Brazil inaongoza 2-1.
0 comments:
Post a Comment