Mahakama ya haki za binadamu
barani Ulaya imeamrisha kuendelea kutekelezwa hukumu ya kupiga marufuku
vazi la hijab linalofunika uso mzima nchini Ufaransa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke mmoja mwenye
umri wa miaka ishirini na nne raia wa Ufaransa ambaye alidai kuwa
marufuku hiyo inakiuka haki zake za kuabudu na kujieleza.Mahakama hiyo hata hivyo imesisitiza kuwa Ufaransa inayo haki ya kuhifadhi utangamano na usawa katika jamii kwa kuweka marufuku hiyo.
Sheria hiyo iliwekwa nchini Ufaransa miaka minne iliyopitana tangu hapo Ubelgiji imeiga.
0 comments:
Post a Comment