Monday, 7 July 2014

MAN UNITED :RASMI YAANIKA JEZI ZAKE MPYA,MSIMU UJAO

RASMI klabu ya Manchester United imetambulisha jezi zake za msimu ujao 2014/15. 

Wayne Rooney alikuwa katikati ya picha, pamoja na wachezaji wenzake Uwanja wa Old Trafford akina Robin van Persie na Shinji Kagawa. 
United inazindua jezi mpya zilizobuniwa na Nike, huku tayari imekwishaingia Mkataba na kocha mpya, Louis van Gaal anayeanza kazi msimu ujao. 

Mwonekano mpya: Manchester United imetambulisha jezi zake mpya

"Zama mpya, jezi mpya. Hivi ndivyo ambavyo Man United ya Louis van Gaal itaonekana 2014/15," wameposti United katika ukurasa wao wa Twitter. 
Rooney na wenzake watavaa jezi hizo kwa mara ya kwanza baadaye mwezi huu watakapokwenda kumenyana na LA Galaxy nchini Marekani katika sehemu ya ziara zao za kujiandaa msimu mpya.

Related Posts:

0 comments: