
Lina Kessy
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ameteuliwa kuwa
Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).
Uteuzi huo umefanywa na
Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma, na Lina
atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao makuu ya
AU yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.
Lina ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) amewashukuru wote
ambao kwa michango yao ya hali na mali imemwezesha kufika hapo.
Ameishukuru TFF kwa kumlea na
kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali kupitia Kurugenzi ya
Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC).
TFF inampongeza kwa uteuzi huo,
na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania ikiwemo kuwa chachu
ya maendeleo ya michezo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment