HATIMAYE mshambuliaji Lionel Messi amesaini Mkataba mpya Barcelona ambao unamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani, akimpiku Mwanasoka Bora wa Dunia kwa sasa, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Pamoja
na hayo, Barcelona imetangaza kumsajili kipa wa gharama kubwa,
Mjerumani Marc-Andre Ter Stegen kutoka Borussia Monchengladbach.
Barca
imeamua kujiimarisha baada ya kumaliza msimu vibaya bila taji chini
ya kocha Martino, ikitolewa katika Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya
na Atletico Madrid ambao pia waliwazidi kete katika mbio za ubingwa wa
La Liga siku ya mwisho.
Nyuso za furaha: Lionel Messi akisaini Mkataba mpya na Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu
Kwa
mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Hispania, Messi atakuwa analipwa
mshahara wa rekodi mpya duniani ya Pauni Milioni 16.3 kwa mwaka na
amejifunga na klabu hiyo hadi mwaka 2018.
Messi
amefunga mabao 28 katika mechi 31 za ligi msimu huu alizoichezea Barca
ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye Primera Division na jumla
amefunga mabao 41 katika mashindano yote msimu huu.
0 comments:
Post a Comment