, YANASA WENGINE WAWILI HATARI
SIKU chache baada ya kumsajili kiungo Zubery Dabi, uongozi wa Ruvu Shooting umekamilisha usajili wachezaji wengine wawili, kiungo Juma Mpakala na straika Chagu Chagula ikiwa ni sehemu ya mkakati wao mkali wa kukisuka kikosi chao kama ilivyoagizwa na kocha mkuu Tom Olaba.
Wiki
moja baada ya kuweka wazi kwamba wachezaji sita wa kikosi cha kwanza
watatemwa kutoka na utovu wa nidhamu na kushuka kwa kiwango, timu hiyo
mwishoni mwa wiki juzi ulimsajili kiungo fundi Dabi kutoka Kagera Sugar.
Masau
Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting, ameiambia BIN ZUBEIRY jijini Dar es
Salaam leo kuwa mwishoni mwa wiki Mkapala na Chagula, wakiwa ni
wachezaji huru, walisaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja kuitumikia
timu hiyo kwenye makao makuu ya klabu hiyo zilizopo Mlandizi, Pwani.
"Tuko katika mchakato mkali na mkubwa wa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ili tufanye vizuri msimu ujao," amesema Bwire.
Mbali
na kuwatumikia mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar
tangu mwaka 2008 hadi msimu huu, Mpakala ambaye ni kiungo mshambuliaji,
aliwahi kuichezea Ashanti United msimu wa 2007/8.
Chagula,
mshambualiji wa Kitanzania aliyekuwa akiichezea timu ya Muzinga ya
Burundi na kabla ya kwenda Burundi, aliwahi kucheza katika timu za
Twiga, Kahama United na Ashanti United hadi mwaka 2007 alipotimkia
nchini humo na kujiunga na timu ya Vital'O aliyoitumikia hadi 2009.
2010
hadi 2011 Chagula aliichezea timu ya Inter Star ya Burundi kabla ya
kuijunga na Muzinga 2012 ambayo ameitumkia hadi msimu huu mkataba wake
ulipomalizika.
"Kwa mujibu wa ripoti na mapendekezo ya kocha
Olaba,
tumbakisha kusajili mchezaji mmoja, beki wa kati. Tunafanya usajili
makini ili tutwae taji la Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao," amesema Bwire
zaidi Bwire.
Aidha,
uongozi wa Ruvu Shooting umekivunja kikosi chake cha pili cha wachezaji
wenye umri chini ya miaka 20 na kutangaza majaribio kwa vijana wenye
umri huo yanayoendelea kwa wiki mbili tangu Mei 15 hadi Mei 28 mwaka huu
klabu hapo.
![]() |
Kocha wa Ruvu Shooting, Mkenya Thom Olaba timu yake imeendeleza usajili wa wapya kwa ajili ya msimu ujao |
Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment