HATIMAYE Manchester United imteua Louis van Gaal kuwa mocha wake mpya baada ya kumfukuza David Moyes mwezi uliopita.
Mholanzi
huyo amesaini Mkataba wa miaka mitatu wa kazi Old Trafford, na
atasaidiwa na Ryan Giggs - ambaye ametangaza kustaafu soka.
Frans
Hoek na Marcel Bout wanajiunga na klabu hiyo kama
makocha wengine wasaidizi, wakati Van Gaal - ambaye kwa sasa ni mocha wa
Uholanzi anakuwa kocha wa kwanza wa kigeni katika klabu hiyo - ataanza
kazi baada ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Mtaalamu
wa Kihoanzi: Van Gaal ataanza kazi Man United baada ya kumaliza
kuiongoza Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwezi ujao
Miezi 12 tangu Sir Alex Ferguson astaafu ukocha wa klabu hiyo, Van Gaal anaanzisha zama mpya katika mtindo mpya.
"Yalikuwa
matarajio yang wakati wore kufanya kazi katika Ligi Kuu ya England.
Kufanya kazi kama mocha wa Manchester United, klabu kubwa duniani,
inanifanya nijivunie sana,"alisema.
WASIFU WA LOUIS VAN GAAL...
Kuzaliwa: Agosti 8, 1951
Umri: Miaka 62
Alipozaliwa: Amsterdam, Uholanzi
Klabu alizochezea: Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam, AZ Alkmaar
Idadi ya mechi alizocheza: 333
Idadi ya mabao aliyofunga: 34
Klabu alizozifundisha: Ajax, Barcelona (two spells), AZ Alkmaar, Bayern Munich
Timu za taifa alizofundisha: Uholanzi (2000-02 na 2012-hadi sasa)
Mataji aliyoshinda akiwa kocha: Eredivisie
(Ligi Kuu Uholanzi,1993-94, 1994-95, 1995-96, 2008-09), Kombe la UEFA
1991-92, Ligi ya Mabingwa Ulaya 1994-95, Super Cup ya UEFA (1995 and
1997), La Liga (Ligi Kuu Hispania,1997-98 na 1998-99), Copa del Rey
(Kombe la Mfalme Hispania, 1997-98), Bundesliga (Ligi Kuu Ujerumani
2009-10
0 comments:
Post a Comment