Monday, 14 July 2014

EVRA KWENDA JUVE BADO MVUTANO, MANGALAKUTUA MAN CITY, NA ZAHA AITAKA PALACE!


SOMA ZAIDI:
MAN UNITED YAITAKA JUVE IONGEZA DAU KWA EVRA!
Mabingwa wa Italy Juventus wameambiwa na Manchester United kuwa wanapaswa kuongeza Dau lao ikiwa wanamtaka Fulbeki Patrice Evra.
Man United wanataka Juve ilipe Pauni Milioni 4 ili waweze kumlipa Evra haki yake kama malupulupu yake kwa kuichezea Man United kwa Miaka 8 ambayo ni Pauni Milioni 1.5.
Hata hivyo, kuna baadhi ya ripoti zinazohusisha kwenda Evra huko Juve na nia ya Man United kumnunua Kiungo wa Juve Arturo Vidal.
Hadi sasa Klabu hizo mbili hazijatoa tamko lolote.
MANGALA KWENDA ETIHAD!
Eliaquim-MangalaSentahafu wa France Eliaquim Mangala ameripotiwa kufuzu upimwaji afya yake Klabuni Manchester City na wakati wowote Uhamisho wake wa Euro Milioni 48 utakamilika.
Mangala, mwenye Miaka 23, anachezea FC Porto ambayo tayari imeshamuuza Fernando kwa Man City Mwezi uliopita kwa Euro Milioni 15.
Mangala alikuwemo kwenye Kikosi cha France chini ya Kocha Didier Deschamps' kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil lakini hakucheza hata Mechi moja.
NEWCASTLE KUMNASA CABELLA
Newcastle United wako mbioni kukamilisha Uhamisho wa Kiungo wa France Remy Cabella anaechezea Montpellier.
Habari hizi zimetobolewa na Kocha Mkuu wa Montpellier Rolland Courbis ambae amesema mazungumzo yamefikia hatua ya mbali.ZAHA-MAN_UNITED
Cabella, mwenye Miaka 22, alikuwemo kwenye Kikosi cha France chini ya Kocha Didier Deschamps' kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil lakini hakucheza hata Mechi moja.
ZAHA AITAKA PALACE IMNUNUE!
Wilfried Zaha ameiomba Crystal Palace imnunue kutoka Manchester United.
Zaha alinunuliwa kutoka Crystal Palace na Meneja aliestaafu Sir Alex Ferguson Miezi 18 iliyopita kwa Dau la Pauni Milioni 20.
Lakini wakati Man United ipo chini ya Meneja alietimuliwa David Moyes, Mchezaji huyo alipelekwa kwa Mkopo huko Cardiff City.
Hivi sasa Palace inataka kumchukua Zaha kwa Mkopo lakini Man United inataka imuuze moja kwa moja na wako tayari kuchukua hata Pauni Milioni 10.

0 comments: