STAA wa Juventus Arturo Vidal ameliambia Gazeti moja huko Nchini kwao
Chile kwamba hakuna Mtu ambae hatafurahishwa ikiwa Manchester United
inamtaka.
Hivi sasa Man United inadaiwa kutaka kumnunua Kiungo huyo ambae alicheza vizuri huko
Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiwa na Chile na Dau lake linatajwa kufikia Pauni Milioni 35.
Vidal aliliambia Gazeti la El Mercurio: “Nimesikia uvumi huu lakini sitaki kuongelea. Kwa sasa nipo vakesheni na nikirudi Italy tutaona.”
Aliongeza: “Manchester United? Nimepoa lakini ukweli nani hatapendezewa ikiwa moja ya Klabu kubwa Duniani inamtaka?”
PAULINHO KWENDA JUVE KWA PAUNI £20M
Gazeti la Uingereza The Sunday Telegraph limedai Juventus wana mpango wa kutoa Ofa ya Pauni Milioni 20 ili kumnunua Kiungo wa Tottenham Paulinho ikiwa Arturo Vidal ataondoka.
Habari hizi zinaonyesha Dili ya Man United na Juve kuhusu Arturo Vidal huenda ikakamilika na ndio maana Juve wanasaka mbadala wake.
Hata hivyo, inadaiwa Tottenham itataka Dau lifikie Pauni Milioni 25 ili imwachie Kiungo huyo wa Timu ya Taifa ya Brazil.
Paulinho alijiunga na Tottenham Mwaka Jana kwa Dau la Pauni Milioni 17 lakini alipoingia Meneja wa Muda, Tim Sherwood, Mchezaji huyo alitupwa Benchi.
Hivi sasa Tottenham inae Meneja mpya Mauricio Pochettino alietokea Southampon.

0 comments:
Post a Comment