TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA RAHABU KIHANIKU (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA MUDA
MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU KWA
MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.343 CMQ AINA YA HONDA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NDULA MWASANGAJA (32) MKAZI WA MTAA WA BAGAMOYO –TUKUYU.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE
30.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA
KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO MTOTO
ANGEL OSWARD (02) MKAZI WA KIKOTA ALIYEKUWA AMEBEBWA NA MAREHEMU
AMEVUNJIKA MGUU WA KUSHOTO NA AMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA –
TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA MAENEO
YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA
WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 19-20
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
30.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:14 USIKU KATIKA MTAA WA MBILINYI – SAE, KATA
YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
TAARIFA ZA MISAKO:
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI. WATUHUMIWA
HAO NI PAMOJA NA 1. JELY EVARIST (24) MKAZI WA MWANJELWA 2. STAFORD
NGENZI (21) MKAZI WA MWANJELWA, 3. ALAN AGUSTINO (23) MKAZI WA ILEMI 4.
ASIFIWE ABSOLOM (22) MKAZI WA JUA KALI 5. DATI SAMWEL (24) MKAZI WA
MWANJELWA 6. MWAKISYE NAZARETH (23) MKAZI WA MWANJELWA NA 7. MICHAEL
EZEKIEL (40) MKAZI WA NZOVWE.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA
MAENEO TOFAUTI JIJINI MBEYA WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 429.
MSAKO ULIFANYIKA KATIKA MAENEO YA JUA KALI, MAKUNGULU NA MAJENGO MAPYA,
KATA ZA ILEMI NA NZOVWE, TARAFA ZA SISIMBA NA IYUNGA MNAMO TAREHE
30.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:30. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA
BHANGI.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA
TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA
NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment