MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DANIEL JOSEPH (20) FUNDI REDIO, MKAZI WA MTAA
WA MWAKA WILAYANI MOMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKIMTUHUMU KUWA NI MWIZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA
12:00 MCHANA KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA.
MAREHEMU ALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA
KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA
ZA JADI MAWE, FIMBO NA RUNGU NA KUOKOLEWA NA ASKARI POLISI WA DORIA.
CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA DECK. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA SILAHA/BUNDUKI MBILI AINA YA GOBOLE ZENYE NAMBA CH 777 NA CH 1031.
SILAHA HIZO ZILIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA KITONGOJI CHA MTAKUJA, KIJIJI CHA MWIJI, KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. AIDHA, WATUHUMIWA WAWILI WAWINDAJI HARAMU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SURUALI MWAIKONYOLE NA SAMSON TUNTUMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MWIJI WALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOSEPH PETER (55) NA 2. DAIMON MWALUKASA WOTE WAKAZI WA ITEZI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA SABA [07].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Post a Comment