Friday, 13 June 2014

PAUNI 150,000 KWA WIKI YA MFANYA SAGNA KUTUA MAN CITY KUTOKA ARSENAL:

 
MCHEZAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Bacary Sagna amejiunga na Manchester City kama mchezaji hurt kutoka wapinzani wao wa Ligi Kuu ya England, Arsenal.
Beki huyo aliyedumua Arsenal kwa miaka saba, amesaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu, ambao utamfanya awe analipwa Pauni 150,000 kwa wiki mbali ya posho.
Baada ya kumalizana na klabu hiyo, beki huyo wa pembeni sasa atajiunga rasmi na City Jula 1 - baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia.
Kimeeleweka: Bacary Sagna amejiunga na Manchester City kwama mchezaji huru kutoka Arsenal

Related Posts:

0 comments: