INGAWA Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema itatangaza kesho mchana uamuzi wa Rufaa ya Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura, lakini habari zisizo rasmi zinasema gwiji huyo amerudishwa kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.
Wakili
Julius Lugaziya ameuambia mtandao huu jioni hii kwamba; “Tumemaliza,
lakini tutakuwa na mkutano kesho mchana kutangaza uamuzi, kwa sasa
huwezi kupata habari yoyote, tumekubaliana hivyo, yote yatatajwa
kesho,”.
Majibu
kama hayo yametolewa pia na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF,
Boniface Wambura Mgoyo, aliyesema; “Uamuzi kuhusu rufani ya Michael
Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais wa Rais utatangazwa kesho
(Juni 11 mwaka huu) saa 6 kamili mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya
Rufani ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Julius Lugaziya,”.
Lakini
kwa mujibu wa habari za kiuchunguzi ambazo MTANDAO HUU imezipata ni
kwamba baada ya mlolongo wote tangu jana Saa 5:00 asubuhi hoteli ya
Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya leo, Wajumbe wa Kamati
hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya
tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba SC. Wambura alikata
rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua
katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo
unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Kamati
ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro
ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA
kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
![]() |
Ni michael wambura akiwa baadhi ya wanachama wa simba pamoja na mashabiki picha na maktaba |
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
kutoka binzubery blog
kutoka binzubery blog
0 comments:
Post a Comment