Tuesday, 10 June 2014

KURA ZA KUTUMIKA KUMRUDISHA WAMBURA KUGOMBEA SIMBA ?





Mgombea wa urais wa Simba aliyekuwa ameondolewa na kamati ya usajili, huenda akarudi.

Taarifa zinaeleza wajumbe wa kamati ya rufaa ya TFF, ngoma imekuwa ngumu kuhusiana na Michael Wambura.

Habari kutoka ndani zinaeleza kutokana na mvutano kuwa mgumu, wajumbe wameona uamuzi wa kupiga kura.

Uamuzi wa kupiga kura unaonekana kumpa Wambura nafasi ya kurudi kwa kuwa wajumbe watatu wako tayari arudi na wawili wanapinga.

Hata hivyo hakujawa na uthibitisho wa kutosha kuhusiana na hilo.

Lakini mtu mmoja wa karibu na Wambura, amezungumza MTANDAO HUU  na kusema: “Mambo mazuri, subiri kidogo.”

Basi ndiyo hivyo, tunaendelea kusubiri wakati kikao hicho kinaendelea.
CHANZO Salehe jembeblog

Related Posts:

0 comments: