TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI KATIKA
KIJIJI CHA IDIGA, KATA YA USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA
YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIMKODI
MWENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.773 CDJ AINA YA T-BETTER
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IMANI EMANUEL (19) MKAZI WA KIJIJI CHA SONGWE
NA WALIPOFIKA MBELE ZAIDI NDIPO ALIJITOKEZA MTU MWINGINE NA KWA PAMOJA
WALINYANG’ANYA PIKIPIKI NA KISHA KUMFUNGA MIKONO NA MIGUU KWA MIPIRA NA
KUTOWEKA NA PIKIPIKI HIYO.
MWENDESHA
PIKIPIKI HUYO ALIFANIKIWA KUJIFUNGUA NA KUKIMBIA KUOMBA MSAADA KWA
WAENDESHA PIKIPIKI WENZAKE NA WANANCHI WA ENEO HILO NA KUANZA
KUWAFUATILIA WATUHUMIWA HAO KISHA KULIZINGILA ENEO HILO NA KUFANIKIWA
KUWAKUTA WATUHUMIWA WAKIIKOKOTA PIKIPIKI HIYO MARA BAADA YA KUISHIWA
MAFUTA. MTUHUMIWA MMOJA KATI YA WAWILI ALIKAMATWA NA KUPIGWA SEHEMU ZA
KICHWANI HALI ILIYOSABABISHA KIFO CHAKE, AIDHA MTUHUMIWA MWINGINE
ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA KUINGIA KATIKA DIBWI LA MAJI NA KUTOKOMEA HUMO.
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MADAWA JASTON (29) MKAZI WA KIJIJI CHA
ISANGATI ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI, USONI NA MIGUUNI NA MUME
WAKE AITWAYE JOSEPH JOHN (49) MKAZI WA KIJIJI CHA ISANGATI.
MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA NDANI YA NYUMBA ALIMOKUWA AMELALA MAREHEMU MNAMO
TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI. TUKIO HILO LIMETOKEA
KATIKA KIJIJI CHA ISANGATI, KATA YA IHANGO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA
YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA
KABLA YA KUTEKELEZA TUKIO HILO ALIMVAMIA NA KISHA KUMCHOMA KISU MKE
WAKE AKIWA AMELALA NDANI KISHA KUKIMBIA. CHANZO CHA TUKIO BADO
KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
WATU
WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. RASHID MFINANGA NA 2. GODENI
KATEMU (60) MKAZI WA UYOLE WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA MAGARI
MAWILI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA NA KISHA KUPINDUKA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI KATIKA
ENEO LA KIJIJI CHA ITEWE, KATA YA INYALA, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA
KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
KATIKA
AJALI HIYO, GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.254 BFZ AINA YA MITSUBISHI
FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RASHID MFINANGA (37) MKAZI WA
MOSHI LIKITOKEA UYOLE KUELEKEA NJOMBE LILIGONGA UBAVUNI GARI T.837 ATC
AINA YA TOYOTA HAICE LILILOKUWA LIKITOKEA CHIMALA KUELEKEA MBEYA MJINI
LIKIENDESHWA NA DEREVA MRADI CHANDE (34) MKAZI WA KIJIJI CHA ILONGO
KISHA MAGARI YOTE KUPINDUKA
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU WANNE WALIJERUHIWA AMBAO MAJINA YAO BADO
KUFAHAMIKA KATI YAO WANAUME WATATU NA MWANAMKE MMOJA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MTOTO
MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JOSHUA SHUKRANI
MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA WALA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 11.06.2014 MAJIRA YA SAA 12:15 MCHANA KATIKA
ENEO LA MTAA WA MWAFUTE, KATA YA ILEMI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TRANSFORMER JIJINI MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA
BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment