Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976
ZIMEBAKI saa chache kuwapokea
washambuliaji wawili wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa katika klabu
ya TP Mazembe ya nchini demokrasia ya Congo, Mbwana Ally Samatta na
Thomas Emmanuel Ulimwengu.
Kuwasili kwa nyota hawa wawili
kumefufua matumaini kwa benchi la ufundi na jana kocha mkuu Mart Nooij
alisema kuongezeka kwa Samatta na Ulimwengu kumekifanya kikosi chache
kiwe na nguvu zaidi katika safu ya ushambuliaji.
Wanandinga hao wa Tanzania jana
waliichezea TP Mazembe katika mechi ya kwanza ya makundi ya ligi ya
mabingwa barani Afrika dhidi ya El Hilal Omdurani ya Sudan na kupigwa
bao 1-0 ugenini.
Licha ya uchovu wa mchezo huo na
safari waliyoianza leo asubuhi, haitawazuia kuitumikia timu yao ya taifa
ya Tanzania, Taifa stars katika mchezo muhimu wa kesho dhidi ya
Zimbabwe.
Taifa stars inahitaji kufunga magoli mengi katika mchezo wa kesho ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Kwa muda mrefu sasa Stars imekuwa
ikivurunda, lakini kuja kwa kocha mpya kunawafanya watanzania wawe na
hamu ya kufuatilia nini kitatokea.
Nooij ameiongoza Stars katika
mechi moja tu dhidi ya Malawi kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya na
kutoka suluhu ya bila kufungana, lakini mechi ya kesho ni ya kwanza ya
kimashindano kuiongoza timu ya taifa ya Tanzania.
Kila mtu ana hamu kuona mfumo wake
wa uchezaji na jinsi atakavyowatumia wachezaji wa Stars ambao jana
aliwasifu kuwa na vipaji vikubwa na uzoefu katika mashindano ya
kimataifa.
Nooij alisema katika mchezo huo
hawatacheza kwa kushindana mithiri ya vita dhidi ya Zimbabwe, bali
wataingia na kucheza mpira kama walivyojiandaa.
Ili Taifa stars ifanye vizuri
kesho, kuna baadhi ya mambo yanatakiwa kuzingatiwa na wachezaji. Najua
wamefundishwa, lakini kilichobaki ni kuyatekeleza kwa nidhamu ya
kimpira.
Mosi; Wachezaji wetu watatakiwa
kuwa shupavu, kucheza kwa kasi, kuzuia kufungwa, na kucheza kwa weledi
mkubwa kwasababu nidhamu ya kimchezo ya wapinzani wao ni kubwa na wana
watu wanaoweza kuamua matokeo wakati wowote akiwemo mshambuliaji hatari,
Knowledge Musoma.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment