MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 31 May 2013

WABUNGE WA DRC WAMSIFU RAISI KIKWETE KWA JITIHADA ZAKURETA AMANI

PictureL-R: Marais J. Kabila na J. Kikwete
Kufuatia wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu, wabunge hao wa Kivu Kusini na Kaskazini wameomba kuwe na 
mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini Congo.

Wabunge wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na makundi ya waasi wanayopingana nayo.

Wabunge wa Kivu wametaka pendekezo la Rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani ya kudumu kwenye eneo hilo.

Mbunge wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.

Akisema “Rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali kupitia mtizamo ulio thabiti. Bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.

Kwa muda wa siku tano sasa pendekeo hilo la rais Kikwete limeendelea kuzusha maoni mengi kwenye vyombo vya habari ngazi ya kisiasa, na kwa watu wa kawaida huko mjini Kinshasa.

---
via Sauti ya America, VOA

Source: 

MOURINHO ASAINI RASIM CHELSEA FOOTBALL CLUB



JOSE MOURINHO ni boss mpya wa Chelsea — na hiyo ni rasmi kwa mujibu wa gazeti la The Sun! 
 http://static.guim.co.uk/sys-images/Football/Pix/pictures/2013/5/1/1367424140498/A-Chelsea-banner-appealin-008.jpg
The Special One ameripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya £40million jana usiku. 

Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa juu wa Chelsea: “Ni rasmi Jose ni kocha wetu tena! Kila mtu anafurahia ujio wake - klabu, wachezaji na mashabiki. 

“Tayari tunajiaandaa na msimu ujao - tuna uhakika utakuwa msimu mzuri sana.”
 
Mechi ya kwanza ya Mourinho inatarajiwa kuwa kwenye mechi ya mataarisho nchini Thailand dhidi ya  Singha All Stars XI, katika ziara ya huko Malaysia na Indonesia. 

Baada ya hapo The Blues wataenda Marekani kwenye michuano ya  International Champions Cup itakayohusisha timu za Real Madrid na Inter Milan, pia Everton, Juventus, AC Milan, Valencia na LA Galaxy.

VIBAKA WAZUA MAJANGA WAM CHOMA MOTO KIJANA MMOJAN MKOANI LINDI

KIJANA ALIYECHOMWA MOTO NA VIBAKA AKIWA HOSPITALINI


KIJANA ISMAIL MAYOBA 31 ANAYE FANYA KAZI BAA YA MANGROV MKAZI WA JAMHURI MANISPAA YA LINDI AMBAYE AMENUSULIKA KIFA BAADA YA KUVAMIWA NA VIBAKA WALIOTAKA KUMPOLA HATIMAE KUMCHOMA MOTO AMELAZWA KATIKA HOSPTALI YA SOKOINE MJINI HUMO

HOFU YA UGONJWA WA KIMETA NCHINI TANZANIA, MIFUGO YAKATAZWA KUINGIZWA ROMBO

Friday, May 31, 2013

K'NJARO UPDATE: HOFU YA KIMETA, MIFUGO YAKATAZWA KUINGIZWA ROMBO



http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/16/Rombo.svg/200px-Rombo.svg.pngSERIKALI imeweka zuio la mifugo kutoka nchini Kenya na maeneo mengine ya Tanzania kuingizwa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro kutokana na hofu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kimeta unaoshambulia wanyama kama ng’ombe.

Mbali na zuio hilo, pia serikali imepiga marufuku uchinjaji wa nguruwe ambao wanadaiwa kulishwa chakula chenye sumu aina ya polad ambao tayari wamesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wanne kulazwa.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Elinas Parangyo, alisema hivi karibuni kuwa nguruwe wengi wamekufa na kwamba uchunguzi uliofanywa na wataalamu kutoka jijini Arusha umegundua sababu ya vifo hivyo ni chakula walichokuwa wakipewa.

“Tulipata tukio la kimeta ndani ya wilaya na daktari wa mifugo aliyesajiliwa alipiga karantini ya kutochinja hovyohovyo kama nyama haijapimwa na wataalamu na hiyo inahusu mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe,” alisema Parangyo.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha zaidi ya nguruwe 70 wamekufa na kwamba licha ya zuio hilo, wako baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiwasafirisha kwa kificho na kwenda kuuzwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Mwandishi wetu:Rombo  DIXON BUSAGAGA

TAARIFA YA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE, UFAULU WAPANDA KWA ASILIMIA 23.

   

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
 
 
Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu. 

Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. 

Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.

Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

KUDANDIA DALADALA KWA POTEZA MAISHA YA MTU MMOJA ILALA BOMA DAR MUDA HUU

MTU MMOJA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUANGUKA WAKATI AKIJARIBU KUDANDIA DALADALA MAENEO YA ILALA BOMA MUDA HUU

Asubuhi hii ajali mbaya imetokea maeneo ya Ilala Boma na  kusababisha kifo cha abiria huyu ambaye hajatambulika kwa jina mpaka sasa baada ya abiria kutaka kudandia bahati mbaya akadondoka na kupasuka kichwa na kusababisha umauti wake
Wasamaria wema wakisaidia kumpakia kwenye gari kwa kumpeleka hospitalini
Damu ya marehemu ambayo kwa kiasi kikubwa imetoka kichwani baada  ya kupasuka vibaya
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kuondolewa kwenda hospitali
Hii ndio daladala ambayo marehemu alikuwa akitaka kudandia na kudondoka kwa bahati mbaya
Umati wa watu ukishuhudia ajali maeneo ya Ilala Boma 
Askari wa usalama barabarani akichukua maelezo kwa dereva aliyesababisha ajali.PICHA ZOTE NA KRANTZ MWANTEPELE( tunaomba radhi kwa picha zilizo  wekwa)

MATUMIZI MABAYA YA SIMU YAMTUPA GEREZANI MWAKA MMOJA

 


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmjxitUrNqCKkA7E2uO-RBoHXAamMHlJLdzPy3xjApXHdYjCy7jHp8vjo7lIoBsJDivUKWgIXjkg3pTMAmZis0CzHHXoe-CZ59ACLMHoz51R9oxkvR7-CpKJ2JKArf4iQFBjNQ6MOxTSpQ/s1600/razr_phone.jpg
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela, Fundi Mwashi Nassoro Mohamed (25), baada ya kukiri kosa la kutoa taarifa za uongo kwa kampuni za simu alipokuwa akisajili namba zake.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, baada ya mshtakiwa huyo kukiri kutenda kosa hilo Mei 27 mwaka huu.

Hakimu Riwa alisema kutokana na kosa la mshtakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwa viongozi wa serikali na kubainika alisajili kwa majina ya uongo, mahakama imemhumu kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya sh milioni 3.

Kabla ya hukumu hiyo, mshtakiwa aliiomba mahakama imhurumie kwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na kwamba alishawahi kuugua ugonjwa wa figo kwa hiyo aliomba kifungo cha nje ili aweze kujikimu kimaisha.

Baada ya kukiri kosa hilo, Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, alimsomea maelezo ya awali na kuwaeleza maofisa wa polisi ngazi za juu makao makuu, walipata taarifa za kiitelejensia kwamba kuna mtu amesajili namba katika mitandao tofauti na anatuma sms kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP ), Saidi Mwema.

Alieleza baada ya upelelezi iligundulika kuwa namba 0687 521947, 0759 799956 na 0687521948 zilizosajiliwa kwa majina tofauti ya Fadhil Issah, Fadhil Issa na Godfrey Joseph ambazo zilikuwa za mshtakiwa.

Hata hivyo ujumbe wa simu uliotumwa kwa IGP Mwema na Dk. Nchimbi haukuainishwa mahakamani hapo.

JAPAN YA TANGAZA KUSAIDIA TANZANIA MABILIONI

Picture
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma tarehe 30. 5.2013 wakitembelea makumbusho ya karakana ya sayansi ya TOSHIBA iliyoko huko Kawasaki karibu na Tokyo nchini Japan inayohusika na utengenezaji wa injini za treni na vifaa vingine vye elektroniki wakiangalia laptop ya kwanza pamoja na calculator iliyotengenezwa na kampuni hiyo mwaka 1985. Rais Kikwete yupo nchini Japan kuhudhuria mkutano wa tano wa uhusiano wa kiuchumi kati ya Japan na Africa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Japan imetangaza misaada na mikopo ya mabilioni ya fedha kusaidia uchumi na maendeleo ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kugharamia uboreshaji wa miundombinu, ujenzi wa miradi ya barabara, ujenzi wa miradi ya maji, uanzishwaji wa skimu ndogo ndogo za umwagiliaji na uboreshaji wa kilimo cha mpunga.

Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Shinzo Abe ametangaza hatua hizo za kuunga mkono jitihada za maendeleo za Tanzania wakati alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi hao wawili wamekutana ofisini kwa Mheshimiwa Abe leo, Alhamisi, Mei 30, 2013, mjini Tokyo kwenye 
siku ya pili ya ziara ya wiki moja ya Rais Kikwete katika Japan ambako miongoni mwa mambo mengine amealikwa kuhudhuria Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Kujadili Maendeleo ya Afrika wa Tokyo International Conference on African Development (TICAD – V) unaoanza Yokohama, mji wa pili kwa ukubwa katika Japan, keshokutwa, Jumamosi, Juni Mosi hadi 3, 2013 na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi za Afrika na washirika wa maendeleo wa Bara hilo.

Miongoni mwa miradi ambayo Japan imekubali kugharimia ambayo baadhi yake inaendelea kujengwa ama karibu inaanza kutekelezwa ni pamoja na Mradi wa Maji wa Mkoa wa Tabora, Mradi wa Kuboresha Usafiri katika Mkoa wa Dar Es Salaam ambao ni pamoja na kupanuliwa kwa Barabara ya Gerezani na Ujenzi wa Daraja Jipya kwenye barabara hiyo, Mradi wa Kuendeleza Kilimo cha Mpunga nchini na Mradi wa Awamu ya Pili ya Kuongeza Uwezo wa Serikali za Mitaa kwa Njia ya Mafunzo.

Miradi mipya ambayo Japan itagharimia ni pamoja na Mradi wa Kuendeleza Miundombinu, Mradi wa kujenga skimu ndogo za umwagiliaji, mradi wa ujenzi wa barabara ikiwa ni pamoja na kugarimia ujenzi wa barabara
katika milango ya kimataifa ya Mwara, Dodoma na Iringa na Mpango wa 10 wa Kuunga Jitihada za Kupunguza Umasikini.

Wakati wa mazumgumzo hayo, Waziri Mkuu Abe pia ametangaza kuwa Japan itagharamia ujenzi wa barabara za juu kwa juu (fly-overs) kwenye makutano ya barabara za TAZARA na Ubungo, ujenzi wa mtambo wa
kuchakata umeme wa Kinyerezi ambako unatekelezwa kwa mpango wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPF).

Waziri Mkuu Abe pia ameitaka Tanzania na Japan kukamilisha “haraka iwezekanavyo” majadiliano ya kufikiwa kwa makubaliano ya kulinda uwekezaji kati ya nchi hizo mbili ili kufungua njia za uwekezaji zaidi
katika uchumi wa Tanzania kutoka Japan, moja ya mataifa tajiri zaidi duniani.

Mheshimiwa Abe ameiomba Tanzania kuunga mkono jitihada za nchi hiyo kujiunga na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) chini ya mageuzi makubwa yanayotarajiwa kufanyika kwenye mfumo wa Umoja huo.

Rais Kikwete alijibu ombi hilo la Mheshimiwa Abe kwa kusema:
“Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaunga mkono moja kwa moja jitihada za Japan kujiunga na Baraza la Usalama kama mwanachama mwenye kura ya turufu. Unajua msimamo wetu kuhusu jambo hili siku nyingi.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Mei, 2013
 

TAARIFA YA POLISI KUHUSU WATU WALIOFALIKI KATIKA VURUGU ZA GESI MTWARA

 
 Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kutokuwa na hofu juu ya taarifa za kutoaminika na  ambazo hazijafanyiwa uchunguzi zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu idadi ya watu waliofariki katika vurugu zilizotokea mkoani Mtwara.

Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Mtwara Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo Paul Chagonja alisema idadi ya watu waliofariki ni watu watatu mpaka hivi sasa na waliojeruhiwa ni watu kumi na nane tofauti na taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na baadhi ya watu.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Fatuma Mohamed (22), Karimu Shaibu (22) na Mussa Mohamed (28) ambapo mpaka hivi sasa mtu mmoja ndiye aliyebakia katika hospitali ya rufaa ya Ligula akipatiwa matibabu.

Chagonja alisema watu 91 walishafikishwa mahakamani kujibu makosa mbalimbali ikiwemo ikiwemo kuharibu miundominu, kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuchoma nyumba moto.

Alisema zaidi ya watu mia moja wameshajitokeza mbele ya tume iliyoundwa kwa ajili ya kukusanya malalamiko kwa yeyote ambaye anaona hakutendewa haki wakati wa kudhibiti vurugu hizo na endapo upelelezi utabaini kuwepo kwa vitendo viovu sheria itafuata mkondo wake.

Hata hivyo alibainisha kuwa Jeshi hilo litahakikisha linamkamata kila mmoja ambaye amehusika katika vurugu hizo na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

 kwa msaada wa wavuti
blog

Thursday, 30 May 2013

HUJUMA KWENYE MKONGO WA TAIFA UKIONA TOA TAARIFA

PictureMwizi wa mkongo wa mawasiliano amekamatwa akiwa na vipande vya mkongo maeneo ya boko darajani jijini Dar es salaam. 

Matukio kama haya yamekuwa ni vipingamizi katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu.

Kutokana na hali hiyo, sisi kama wadau wa mawasiliano, tunapenda kuwaasa Watanzania kwa ujumla, kama kweli tuna uzalendo wa kweli na mapenzi ya dhati na kampuni yetu ya mawasiliano inabidi  kujitoa zaidi katika kufanikisha usalama wa miundombinu ya kampuni yetu.

Kwa matukio yoyote kama haya naomba msisite kutoa taarifa polisi au toa taarifa kwa namba zifuatazo:- 0737206622 , 0737206623, 0737206624 , 0737206625, 0737206626.

MSEMAJI
OFISI ZA MKONGO WA TAIFA

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2UlZJRnpv

WATU 92 WAFIKISWA KIZIMBANI KWA CHANZO CHA VURUGU ZA GESI MTWARA

Watu 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mtwara na kusomewa mashitaka mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo, kuvunja nyumba, kuiba, kujeruhi na kuhujumu uchumi katika vurugu zilizotekea mjini Mtwara, Mei 22, mwaka huu.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mussa Esanju.
Waendesha Mashitaka wa Serikali, Justine Sanga, na Renatus Mkude, walidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo katika tarehe hiyo. 

Watuhumiwa kwa pamoja walikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande.

Uamuzi huo unatokana na wengi wa washtakiwa kukabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi, kosa ambalo mahakama hiyo haina uwezo wa kuwaachia kwa dhamana.

Hakimu Esanju aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.


Source:  Nipashe gazeti

RAIS J KIKWETE APATA MSAADA WA WAALIMU KUTOKA JAMAICA




RAIS Jakaya Kikwete ameomba msaada wa walimu wa Hisabati na Sayansi kutoka nchini Jamaica ili kukabiliana na upungufu wa wataalam hao nchini.
 
Rais Kikwete alitoa ombi hilo Jumatatu ya juma hili kwenye Hotel ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Jamaica, Mama Portia Simpson Miller.

Ikulu ilisema kuwa Rais Kikwete alikuwa Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Juni 25, 1963 na Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU wakati Mama Simpson Miller alipokuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa nchi mbali mbali duniani walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosambazwa jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa katika mazungumzo ya viongozi hao wawili, Mama Portia Simpson Miller ambaye aliapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica Januari 5, 2012 baada ya chama chake cha Peoples National Party (PNP) kushinda uchaguzi mkuu nchini humo, alimwuliza Rais Kikwete jinsi gani Jamaica inavyoweza kuisaidia Tanzania.

Kutokana na swali hilo, Rais Kikwete aliomba mambo mawili, mosi kupatiwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi pamoja na kocha wa riadha.

Kutokana na ombi hilo, mama huyo alimwahidi Rais Kikwete kuwa Jamaica ina uwezo wa kusaidia katika maeneo yote mawili.

Kutokana na makubaliano hayo, serikali sasa inatarajiwa kupata walimu wa masomo hayo mawili na kocha wa mchezo wa riadhaa. Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja idadi ya walimu wa masomo hayo.

Katika matokeo ya kidato cha nne na sita, kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli masomo hayo kwa madai kuwa walimu wanaoweza kufundisha masomo hayo ni wachache.
Lakini kibaya zaidi wataalam wa masomo hayo licha ya uchache wao, hawana motisha na ndio sababu yao kutofundisha vizuri na kusababisha matokeo mabaya katika masomo hayo.

Mbali ya makubaliano hayo, nchi hizo mbili zimeahidi kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali na kuangalia uwezekano wa Tanzania kufungua aina ya uwakilishi katika Kisiwa hicho cha Caribbean katika miaka miwili ijayo.

Kuhusu kocha wa riadha, Mama Simpson Miller amesema kuwa na hilo halina pingamizi kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Michezo kwa miaka mingi na kuwa kwa sasa Wizara ya Michezo iko kwenye Ofisi yake ya Waziri Mkuu.

Jamaica ni moja ya nchi zinazoongoza katika mchezo wa riadha duniani ikiwa imetoa wanariadha wengi mabingwa wa dunia akiwamo bingwa wa sasa wa Olimpiki na dunia katika mbio fupi za mita 100 na 200, Usain Bolt. 
kwa msaada wa Jaizmilaleoblog

YANGA SC YAMUONGEZA MKATABA NIZAR KHALFAN, YAMUITA MCHEZAJI WA KUIGWA NDANI YA TIMU


  

nizar
Nizar Khalfan katika picha tofauti, mbili kulia akiwa na Yanga SC na kushoto alipokuwa Marekani 
KLABU ya Yanga imesema kwamba, kiungo Nizar Khalfan ataongezewa Mkataba ili aendelee kuichezea klabu hiyo msimu ujao baada ya msimu huu kuuridhisha uongozi na benchi la Ufundi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmad Bin Kleb amenena jana kwamba, Nizar anawavutia hata viongozi kutokana na nidhamu yake ya hali ya juu.
“Yule mchezaji kwa kweli ni mfano wa kuigwa katika suala la nidhamu. Na pia huwa anaonyesha uwezo mkubwa sana anapopewa nafasi. Naweza kusema, katika wachezaji ambao wamemaliza Mikataba, yule ni miongoni mwa waonabaki,”alisema.  
Kuhusu wachezaji wengine waliomaliza mikataba akina Nurdin Bakari, Oscar Joshua, Stefano Mwasyika, Godfrey Taita na kipa Said Mohamed, Bin Kleb alisema hatima yao itajulikana wiki mbili zijazo.
Kuna ripoti mwalimu kaiandika kuhusu timu kwa ujumla, ndani yake kuna wachezaji ambao amesema hatawahitaji tena. Tutaipitia na kwa wale ambao mwalimu amesema atawahitaji tutaagana nao kiungwana na kuwapa asante yao kwa kuitumikia klabu,”alisema.
Bin Kleb alisema wapo wachezaji wengine ambao hata kama hawataguswa na ripoti kocha, lakini uongozi umegundua ni mushkeli katika klabu, nao pia watapewa ‘mkono wa kwaheri’.
Kuhusu usajili, Bin Kleb alisema bado wanaendelea kwa umakini wa hali ya juu na wanafanya hivyo kulingana na mapendekezo ya kocha wao, Ernie Brandts ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni kwao, Uholanzi.
“Usajili unaendelea na kama unavyojua, haya si mambo ya kukurupuka, basi tunafanya taratibu na lengo letu ni kuhakikisha siyo tu tunaendelea kutawala katika soka ya Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, bali pia kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika,”alisema Bin Kleb. 
Yanga ilimsajili Nizar kutoka Marekani msimu huu ambako alikuwa akicheza soka ya kulipwa na katika msimu wake wa kwanza, anajivunia kutwaa mataji mawili, Kombe la Kagame na Ligi Kuu.
Yanga inatarajiwa kuanza mazoezi Juni 3,  mwaka huu kujiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano ambayo itafanyika nchini Sudan mwezi ujao.
Katika michuano hiyo, mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Kagame, wamepangwa Kundi C pamoja na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na Vital 'O' ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Mabingwa watetezi, Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo Juni 20 kwa kumenyana na Express, wakati Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, na mechi zote zitachezwa Elfashar.

KICHANGA CHAUKOTWA NDANI YA BOMBA LA MAJI TAKA KIKIWA HAI…

 

clip_image002 
Mtoto mchanga aliyeokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka nchini China, alianguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya, mamake mtoto huyo amesema.
Mama huyo ambaye bado hajatajwa jila lake, aliambia polisi kuwa alijifungua mwanawe akiwa chooni na kuwa mtoto huyo aliteleza na kuanguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya
Mama huyo anaripotiwa kuangua kilio cha mwanawe , licha ya kuwa hakukubali kuwa ni mwanawe hadi baadaye.
Mtoto huyo anapokea matibabu hospitalini baada ya kuokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka. Bomba hilo lilikatwa kwa ustadi baada ya majirani kusikilia kilio cha
mtoto huyo mjini Jinhua Jumamosi.
Shirika la habari la Zhezhong, lilisema kuwa mamake mtoto huyo mwenye umri wa miaka 22, aliambia polisi kuwa hangeweza kumudu gharama ya kuavya mimba. Hajaolewa na aliiweka mimba yake kuwa siri kubwa.
Alisema kuwa alijaribu kumzuia mtoto wake kuanguka baada ya kujifungua kwa ajali akiwa hospitalini lakini alianguka ndani ya bomba. Hata hivyo alimweleza mpangaji wake kulingana na shirika la habari la Xinhua.
Mama huyo alisema hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe kwa hivyo hakuambia yeyote kuwa ni mwanawe. Hata hivyo baadaye alijitambulisha na kuambia polisi ni mwanawe baada ya kuokolewa kwake.

Polisi wanachunguza ikiwa tukio hilo lilikuwa la ajali au kilikuliwa kitendo cha maksudi.
Mtoto huyo alipatikana ndani ya bomba lenye urefu wa nchi nne
Alipata majeraha madogo kichwani na mikononi lakini anaendea kupata matibabu.
Kisa hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya China huku baadhi wakisema kuwa mtoto huyo alikuwa ametupwa na mamake kwa maksudi.
Sheria za China za kupanga uzazi ni kali mno huku familia ikiruhisiwa kuzaa mtoto mmoja pekee na wazazi wanaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini ikiwa watapatikana na hatia ya kupata zaidi ya mtoto mmoja.

Wednesday, 29 May 2013

SOKA LA HISPANIA NA BLAZLI JE NEYMAR ATAWEZA BARCELONA?


Romário (1993), Ronaldo (1996), Rivaldo (1997), Ronaldinho (2003) na Neymar (2013).
 
Neymar anajiunga ma urithi mzuri wa washambuliaji wa Brazil unaoundwa na wanaume wanne waliopata mafanikio makubwa katika miongo kadhaa iliyopita na kupata mafanikio makubwa ndani ya Nou Camp - sasa ni zamu  Neymar da Silva.

Romário na Ronaldo
Romário aliigusa mioyo ya mashabiki wa Barca kwenye msimu wa 1993-4, wakati alipopewa jina la “cartoon footballer” kutokana na kuwa uwezo mkubwa mno wa kucheza soka. Aliposajiliwa alihaidi kufunga mabao 30 ya ligi na akatimiza ahadi yake huku kikosi cha Cruyff kikishinda ubingwa msimu huo, Romario alirudi Brazil baada ya nusu ya msimu uliofuatia.

Mara baada ya Romario kuondoka kinda la miaka 19 - Ronaldo De Lima aliwasili Camp Nou. Alikuwa na nguvu, mwenye ujuzi na mwenye uchu wa mabao - kwenye msimu wake wa kwanza alifunga mabao 47 kwenye mechi 51.

Rivaldo na Ronaldinho
Wakati Ronaldo alipohamia Inter, Rivaldo akaja Camp Nou akitokea Deportivo. Rivaldo akawa nyota wa kikosi cha Van Gaal kilichoshinda ligi mara mbili. Alifanikiwa kushinda mchezaji wa dunia mwaka 1999.

Kuwasili kwa Ronaldinho mwaka 2003 kukaleta mageuzi makubwa kwa klabu ya Catalunya na kuleta tabasamu lilopotea na mashabiki wa Barca. Baada ya ukame wa miaka mitano bila kombe, aliiongoza Barca kushinda ubingwa wao wa pili wa ulaya jijini Paris na kushinda uchezaji bora wa ulaya na dunia kwa mara kadhaa. 

Evaristo, Giovanni and Anderson
Romário, Ronaldo, Ronaldinho na Rivaldo wanaweza kuwa ndio washambuliaji wa kibrazil waliopata mafanikio makubwa zaidi, lakini hawakuwa wa brazil pekee walioleta sura za furaha Camp Nou. Kwa mfano miaka ya1950s, Evaristo de Macedo alifunga mabao 173 kwenye 219. Miongo kadhaa baadae mwishoni mwa miaka ya 90, Giovanni Silva na Sony Anderson pia walileta sura za furaha Catalunya kwa viwango vyao.

Sasa ni zamu ya Neymar - je atafuata nyayo za magwiji ya Brazil waliomtangulia kucheza Camp Nou na kuwafunika kabisa kimafanikio? Muda utaongea. http://feeds.feedburner.com/%7Er/ShaffihDaudaSportsBlog/%7E4/zcKPblRYQeo?utm_source=feedburner&utm_medium=email
CHANZO: SHAFII DAUDA

MTOTO WA SOKOINE ATAKA MWILI WA BABA YAKE UCHUNGUZWE

 


MTOTO mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine, Lazaro Sokoine, ameibuka na kutoa madai mazito ya kutaka mwili wa baba yake ufanyiwe uchunguzi, kubaini chanzo cha kifo chake.
 http://onafricajournal.com/wp-content/uploads/2011/10/nyerere_and_sokoine.jpg
HAYATI MWALIMU JK NYERERE NA HAYATI EM SOKOINE 
Mbali na kutaka uchunguzi huo, Lazaro pia amemuandikia barua Rais Jakaya Kikwete akielezea mlolongo wa matukio mengi, likiwemo mgogoro wa familia hiyo na kuporwa kwa ardhi na mali zake zingine alizoachiwa na Hayati Sokoine.

Lazaro alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu, huku akishusha madai mazito dhidi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Namelock Sokoine, ambaye ni mdogo wake.

Kwa nini mwili wa Sokoine uchunguzwe?
Akielezea sababu za kutaka mwili wa Sokoine uchunguzwe, Lazaro alisema miezi minne kabla ya kifo chake mwaka 1984 baba yake alienda nchini Cuba wakati Lazaro akiwa masomoni nchini humo; Sokoine alimwambia mwanaye huyo kuwa asishangae kusikia amekufa kwa njia yoyote ile ikiwamo kupigwa risasi kwani kuna watu wanamuwinda.

Alisema baada ya baba yake kumueleza hivyo alihoji sababu ya kuwa na hofu hiyo ambapo Sokoine alijibu kuwa hali ya nchi wakati huo chini ya Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa mbaya kutokana na vita dhidi ya wahujumu uchumi.

Mtoto huyo  ambaye ana hali mbaya kiuchumi, alisema baba yake aliendelea kumwambia kuwa kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere alimuongezea ulinzi kutoka askari wanne hadi 14.

“Baba alikuja Cuba kwa ajili ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo na akaniambia maneno hayo mazito nami nikaenda kuongea na walinzi wake ambao ni Mashaka, Kimaro na Kalbert juu ya hofu hiyo ya baba,” alisema Lazaro.
Alisema miezi minne baadaye alipata taarifa ya kifo cha baba yake kupitia Ikulu ya Cuba hali iliyomfanya ayakumbuke maneno ya tahadhari aliyoambiwa juu ya hofu ya kuuawa.

Akieleza sababu nyingine iliyomfanya atake mwili wa baba yake uchunguzwe upya, Lazaro alisema agizo la Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa wakati huo Imran Kombe, kuwataka walinzi wa Sokoine waliokuwa Dodoma watangulie Arusha badala ya kuandamana naye kwenda jijini Dar es Salaam, linatia shaka kwamba kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua.

Alisema kutokana na mazingira hayo, amekuwa akitamani sana kuanzisha harakati za kutaka mwili wa kiongozi huyo maarufu uchunguzwe, lakini hali yake kiuchumi ndiyo inayomkwamisha.

“Kwa sasa sina uwezo ila nikipata pesa nitaanzisha mchakato wa kuchunguza kifo cha baba yangu; nimekuwa nikiuliza hili kwa muda mrefu, watu wamenichukia na sasa wananipiga vita hadi ndani ya familia kwa kuhoji suala hilo, mdogo wangu anayeitwa Joseph Sokoine aliyeko ubalozi wa Tanzania nchini Canada aliniambia nisiulizeulize hili suala, wala nisiliingilie kwani siku moja wataning’oa macho au kuniondoa duniani,” anaongeza Lazaro.

Alisema hivi karibuni wakati mwili wa Sokoine ulipozikwa kwenye kaburi jipya kutoka lile la awali, aliiambia familia yake kwamba isifunge milango ya kaburi ili uchunguzi wa mwili wa baba ufanyike.

Hivi karibuni gazeti la Tanzania Daima lilipata kuandika taarifa ya mwili wa Sokoine kuzikwa kwenye kaburi jipya baada ya lile la awali kuharibika na kwamba familia ina mpango wa kutaka kuufanyia uchunguzi mwili huo.

Ikumbukwe kuwa wakati wa kifo chake kulikuwa na mjadala mzito, wengi wakidai aliuawa na kwamba kifo chake kilipangwa na mahasimu wake ndani na nje ya serikali ambao walikerwa na operesheni yake ya kupambana na wahujumu uchumi na mali za taifa.

Kwa mujibu wa sheria, mwili ukishazikwa unaruhusiwa kufanyiwa uchunguzi baada ya miaka 30 na mwakani mwili wa Sokoine utafikisha umri wa miaka 30 tangu ulipozikwa na huo utakuwa muda muafaka kwa wana ndugu hao kutaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yao.

WATANZANI MAJONZI KWENYE BONGO FLEVA M TO THE P" NAYE AAGA DUNIA, BAADA YA NGWAIR

TANZANIA BONGO "M TO THE P" NAYE AAGA DUNIA, BAADA YA NGWAIR

BAADA YA MANGWEA SASA NI “M to the P”
Duru za Habari kutoka nchini Afrika Kusini, Baada ya kifo cha Msanii wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva na Hip Hop) Albert Mwangwea a.k.a kijana wa Jakaya, “M to the P” naye afariki dunia nchini humo.
Mangwea amefariki jana Jumanne wa kile kinachodaiwa ni matumizi ya dawa za kulevya kufuatia kuwa na matumizi nayo kwa muda mrefu.
“M to the P” msanii mwingine wa karibu na marehemu ambaye alikutwa amezirai baada ya naye kutumia dawa za kulevya zilizozidi kiasi naye afariki dunia  katika Hospitali ya St. Hellen ya mjini Johannesburg.
Duru nyingine za Habari zinasema huenda wote wawili walikula chakula chenye sumu.  ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO  HUU

BUNGENI DODOMA : SERIKALI YAKIRI KUTOLIPA FIDIA ARUMERU MASHARIKI

 



http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2011/04/Tanzania-Parliament.jpgSERIKALI imekiri kuwa haijalipa fidia kwa wananchi wa Wilaya ya Arumeru ambao walitakiwa kupisha upanuzi wa miradi ya EPZ.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na zoezi la upimaji wa uthamini kutokukamilika.

Teu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) aliyetaka kujua ni lini serikali italipa fidia kwa mashamba ya wananchi wa Malula, Kata ya King’oli baada ya mashamba yao kuingizwa katika mipango ya EPZ.

Akiendelea kujibu swali hilo, Teu alisema Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya EPZ ilibainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 4,000 chini ya Kijiji cha Malula.

Alisema juhudi za kutwaa eneo hilo mwaka 2008 zilianza ambapo EPZ ilituma sh milioni 22 kwenda Halmashauri ya Meru kwa ajili ya uhamasishaji, upimaji na uthamini wa eneo zima.

Naibu huyo alisema kati ya miaka ya 2009 hadi 2011, uongozi wa Wilaya ya Arumeru kwa kushirikiana na Mamlaka ya EPZ ulifanya vikao mbalimbali vya upimaji na uthamini wa eneo husika pamoja na makubaliano ya wamiliki.

Hata hivyo, alisema wananchi hao wanaruhusiwa kuendelea na kazi za kilimo cha mazao ya muda mfupi katika maeneo hayo.

MASHOGA WA KWANZA KUOANA LEO, UFARANSA



Ufaransa  itasherehekea  harusi  ya  kwanza  ya  watu  wa  jinsia moja  leo wakati  Vincent Autin  na Bruno  Boileau  kufunga  pingu  za maisha, siku  chache  baada  ya  sheria  ya  ndoa za  watu  wa jinsia  moja  kuidhinishwa kuwa sheria  kamili hali  iliyozusha maandamano makubwa. 
 http://www.washingtonpost.com/rf/image_606w/2010-2019/WashingtonPost/2013/05/18/Foreign/Images/Par7561778-9608.jpg
Autin , mwenye  umri  wa  miaka  40  na Boileau mwenye  umri  wa  miaka  30, watafunga  pingu  za  maisha katika  harusi  itakayofungwa  na  maafisa  wa  serikali  katika  mji wa  kaskazini  wa  Montpellier.

Meya  wa  jiji  hilo  ambaye  anatoka  katika  chama  cha  Kisoshalist atafungisha  ndoa hiyo  katika  jengo  la  halmashauri  ya  jiji, ndoa ambayo  imepangwa  kufanyika  jioni  ya  leo.

Polisi  watakuwepo  kuzunguka  jengo  hilo, baada  ya  maandamano makubwa  kufanyika  siku  ya  Jumapili  na  watu  wanaopinga  ndoa za  aina  hiyo , ambayo  yaligeuka  baadaye kuwa  ya  vurugu. Kiasi ya watu 350 wamekamatwa   kutokana  na ghasia  hizo mjini Paris.

SIASA ZA BONGO KINANA ATOA ONYO UCHAGUZI 2015

 


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
 http://4.bp.blogspot.com/-oKKghHCoG30/UWzSxSo_XrI/AAAAAAACNd8/Vq6Y_KfuTUk/s640/10.+Kinana+akihutubia+mkutano+wa+hadhara+katika+Kijiji+cha+Mwaya%252C+Ulanga%252C+Morogoro.jpg
Kinana alisema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla  ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo.

Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

Kinana alisema,  kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.

Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25  kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.

KILICHOMUUA NGWEAR CHA FAHAMIKA NA TARATIBU ZA MAZISHI ZAANZA MBEZI BEACH




Taarifa ambazo MBEYAGREENNEWS.BLOGSPORT .COM imezipata kutoka Afrika ya Kusini kwa HusseinOriginal ambaye yupo Pretoria, a
mesema Ngwear amefariki Jana jion kwenye gheto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahtuti. 

"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"

Baada ya kuwapeleka hospitali Daktari alitibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa Karibu wa Ngwear huko Afrika nya Kusini.

Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar jana lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya na M to the P.

Taarifa ya hospitali hii hapa "
The Medical report from Helen Joseph hospital, Dr Shirley Radcliffe confirming that albert Mangwairdied from “alcohol toxicity” after drinking toomuch,Over-exhaustion and drugs overdose....The inquest heard that Albert 28, collapsed in the his friends home had been more thanfive-times the legal S.A drink-drive limit with 416mgof alcohol per 100 milliliters of blood in his system....Radcliffe described the reasons for ICU admission included hypoxia and one of his friend found “two empty vodka bottles[found] on the Car” and he had been suffering from the eating disorder Bulimia for several months before his death and endless partying session with little or no resting...sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he overdosed Heroin,Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in his blood...and his death was caused by massive heart attack and respiratory failure followed by sudden Heart stop...and end up dead within seconds!"

Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.

Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.

 
 
NA  TARATIBU ZA MAZISHI  ZAANZA MBEZI BEACH

FAMILIA ya msanii Albert Mangwea aliyefariki dunia jana nchini Afrika Kusini, imeanza taratibu za mazishi na jioni hii inafanya kikao Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.

Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, alifariki dunia jana jioni akiwa nchini Afrika Kusini 
kutokana na kuzidiwa na matumizi ya dawa za kulevya. Wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St Hellen Joseph, rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali mbaya, pia kwa utumiaji wa dawa za kulevya ambako hadi sasa amelazwa kwa matibabu na taarifa zinasema anaendelea vizuri.
Kaka wa marehemu Ngwair, Kenneth Mangwea amesema msiba upo Mbezi Beach, Goigi mjini Dar es Salaam na taratibu za kuirejesha miili ya marehemu nyumbani zimeanza.

Kimuziki, Ngwair aliibukia mkoani Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Dark Master, Noorah na Mez B na amekuwa akishirikiana na M To The P tangu akiwa msanii anayechipukia baada ya kuhamia Dar es Salaam.

Baada ya kuja Dar es Salaam, Ngwair akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.

Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.

Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.

Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.

Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.

Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.  

Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. 

Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. 

Ngwair alijaribu sana kumuinua kimuziki M, lakini pamoja na ukweli kwamba alikuwa ana kipaji, lakini hakufanikiwa, ingawa aliwahi kutoa albam 

Tuesday, 28 May 2013

MBUNGE WA CCM AMKACHA PINDA

Na Haika Kimaro na Mary Sanyiwa, Mwananchi  (email the author)

 
Waziri Mkuu alitembelea Ofisi ya CCM Mtwara Vijijini, Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya Kata ya Mtonya Mikindani, Ofisi ndogo ya Mbunge (Murji), Baa ya Mukuzi, nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na ya Mbunge wa Mtwara Vijijini.Mtwara. Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji ameikacha ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu zilizotokea mkoani hapa wiki iliyopita.
Katika ziara yake, Waziri Mkuu alitembelea Ofisi ya CCM Mtwara Vijijini, Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya Kata ya Mtonya Mikindani, Ofisi ndogo ya Mbunge (Murji), Baa ya Mukuzi, nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Nyumba ya Mbunge wa Mtwara Vijijini, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia ambazo zilishambuliwa katika vurugu za mwanzo.
Akizungumzia sababu za kukacha ziara hiyo, Murji alisema: “Ni kweli nilialikwa lakini kilichonifanya nisiungane na Waziri Mkuu ni ratiba kutokuonyesha kutembelea maeneo ya wananchi waliopatwa na maafa.
“Ratiba ile ilionyesha Waziri Mkuu atatembelea maeneo ya viongozi na Mahakama pekee bila kutembelea maeneo ya wananchi ndiyo sababu iliyonifanya nisihudhurie, wananchi wasingenielewa. Wangenigeuka na wangeniona nimewasaliti.
“Kwa kuwa nipo upande wa wananchi, nisingeweza kutembelea maeneo ya viongozi wa Serikali pekee lakini kesho (leo) wakati Waziri Mkuu akitembelea walioathirika na mimi nikiwa Mbunge wa Mtwara Mjini nitatembelea maeneo yote ya wananchi wangu waliokumbwa zahama hiyo.”
Murji alisema sababu ya kukataa gesi isitoke ni kutokana na nafasi nyingi za ajira kupatiwa wananchi wa nje kwa asilimia 90 huku asilimia 10 pekee ikibaki kwa wananchi wa Mtwara hali inayowafanya wananchi wasijue ni nini kitakachofuata baada ya gesi kupelekwa Dar es Salaam.
“Ni kweli wawekezaji ni wengi wanataka kuwekeza Mtwara na kama tulivyoelezwa kuna maombi ya wawekezaji 45, viwanda vingi vitakuja lakini ukiangalia upande wa ajira asilimia 90 zote zimeenda kwa watu wa nje,” alisema Murji.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, wakuu wa wilaya za mkoa huo, Kamishna wa Polisi (Operesheni), Paul Chagonja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mohamed Sinani na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Akitoa maelezo ya tathmini ya mali zilizoungua Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mtonya, Yusuph Kaliwanje alimweleza Waziri Mkuu kuwa uchomaji wa majengo hayo ulianza saa nane mchana. Alisema ofisi ya kata hiyo yenye thamani ya Sh32 milioni, ilichomwa moto pamoja na nyaraka mbalimbali na samani.
Pia alisema vibanda mbalimbali vya wafanyabiashara pamoja na mali zilizoharibiwa zina thamani ya Sh33 milioni. Alisema tathmini ya hasara ya Ofisi ya Mbunge bado haijajulikana.


Na Haika Kimaro na Mary Sanyiwa, Mwananchi gazeti  
 

WANAFUNZI WAPIGA KURA KWA SIRI ILI KUBAINI MWL ANAEFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI (SHINYANGA)

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyasubi, iliyopo Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wamepiga kura za siri ili kuwafichua walimu wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi wao shuleni hapo.

Uamuzi wa kupigwa kura hizo ulifikiwa hivi karibuni kwenye Kikao cha Baraza la Shule la Watoto ambacho kiliitishwa kwa lengo la kujadili vurugu zilizokuwa zikijitokeza shuleni hapo na kusababisha baadhi ya walimu kupigwa.

Kikao hicho kiliitishwa na Mratibu wa Mradi wa Haki Yangu Sauti Yangu, mkoani humo, Bw. Gerald Ng’ong’a na 
Kkubaini kuwa, sababu moja wapo iliyochangia vurugu hizo ni baadhi ya walimu kufanya mapenzi na wanafunzi wao.
Inadaiwa hali hiyo pia imechangia wanafunzi wengi waliomaliza kidato cha nne shuleni hapo kupata matokeo mabaya, kuporomoka kwa kiwango cha elimu kutokana na walimu kutotimiza wajibu wao kikamilifu.

Baadhi ya wanafunzi waliozungumza katika kikao hicho, walisema chanzo cha vurugu ni wanafunzi wa kiume kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike hivyo wanachukizwa na kitendo cha baadhi ya walimu kutembea na wapenzi wao.

Walisema kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa kiume waendapo mitaani hujiunga na vikundi vya wahuni ambao huchukua hatua za kuwateka na kuwapiga walimu wao ili kulipa visasi.

Hata hivyo, wanafunzi hao walipotakiwa kuwataja walimu wenye tabia hiyo waliomba ufanyike mchakato wa upigaji kura za siri ambapo kazi hiyo ilisimamiwa na walimu pamoja na wazazi walezi ambao walishiriki kikao hicho.

Kura hizo ziliwataja majina ya baadhi ya walimu wenye tabia hiyo na majina ya wanafunzi wanaoshiriki kufanya nao mapenzi lakini hazikutangazwa kwa kuwa ni siri na zitawasilishwa kwa uongozi wa shule ili wahusika waitwe na kuonywa.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wanafunzi shuleni hapo walilalamikia kitendo cha walimu wao kuwapa adhabu kubwa zisizolingana na makosa wanayoyafanya wakitolea mfano wa adhabu ya kugaragazwa chini kwa kosa la kutokutoa ada ambalo walisema si kosa lao bali ni la wazazi.

Kutokana na hali hiyo, Bw. Ng’ong’a, aliwashauri wazazi, walezi kuhakikisha wanafanya vikao vya mara kwa mara ili waweze kurejesha hali ya amani na utulivu shuleni hapo.

"Nimesikitishwa kusikia miaka minne hamjaitisha kikao chochote cha Bodi ya Shule wala cha wazazi, hali hii inachangia mambo mengi kutopatiwa ufumbuzi wa haraka pale yanapojitokeza.

"Ni muhimu kuwa na vikao vya mara kwa mara pamoja na Baraza la Shule la Watoto ili kutoa fursa ya kusikiliza kero mbalimbali walizonazo," alisema Bw. Ng’ong’a.


---
Imeandikwa na Suleiman Abeid, Kahama


MHUBIRI ALA KICHAPO KIKALI MARA BAADA YA CONDOM KUDONDOKA IKITOKEA KWENYE BIBLIA

 


HALI tete na ya taharuki imezuka katika jiji la LAGOSI huko Nchini Nigeria mara baada ya Mwinjilisti mmoja aliyejulikana kwa jina la Mr John Mbakogwu.

Mr John Mbakogwu aliushangaza umati mkubwa ambao walikuwa ndani ya basi hilo wakisafiri kulekea maeneo mbali mbnali na kuacha taswira ambbayo haikuweza kueleweka kwa haraka kutokana na Mr John Mbakogwu kuonekana akihubiri kwa hisia kali huku akiwasisitiza wanajamii kuacha Dhambi kwa siku za mwisho zimefika.

Wakati akiendelea kutoa neno la Mungu Ghafla Condom ambayo alikuwa ameihifadhi ndani ya kitabu kitakatifu cha BIBLIA ndipo ilipoanguka chini huku abiria waliokuwa wakionekana wakiguswa na mahubiri ya mhubiri huyo wakishuhudia kwa macho yao na kubaki wakishanga kwa kutoamini lililotokea. Ndipo waumini hao waliposhikwa na hasira na kuanza kumshambulia kwa kumchapa makonde ya Nguvu na mwishowe raia wema ndipo walipoamua kumgombelezea kutoka kwenye Umati huo wa waumini wenye hasira na hivyo kufanikiwa kusalimisha uhai wake huo ambao ulionekana kuwa rehani .
Yo

SELIKALI IANGALIE USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI WAWAPO KAZINI


Kajubi MukajangaKATIBU Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga, ameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuchukua hatua za ziada za kuwahakikishia waandishi wa habari usalama wawapo kazini.

Mukajanga alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumzia vurugu za masuala ya gesi zilizoibuka wiki iliyopita mkoani Mtwara.

Alisema MCT inasikitishwa na kilichojiri mkoani humo hasa wananchi kupoteza maisha, mali kuharibiwa vibaya na amani kutoweka huku maisha ya baadhi ya waandishi wa habari yakiwa hatarini.

Alisema baraza hilo lilizungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Serikali ya Dailynews na HabariLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Standard Newspapers (TSN) Ltd, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Uhuru na Mzalendo ambao katika vurugu hizo pamoja na kuharibiwa mali zao walilazimika kukimbilia mafichoni kuokoa maisha yao.

Aliwataka wananchi kutambua kwamba kazi ya uandishi wa habari ina misingi yake.

“Jamani si kila kitu kinaandikwa au ni habari sasa hawa walishambuliwa eti kwa sababu tu hawakufanya yale ambayo wananchi wanayataka hii si sahihi, mbona mkulima wa karanga akilima mahindi hashambuliwi kwa kufanya tofauti.”

Aliiomba Serikali iweke utaribu mzuri wa kuhakikishia waandishi wa habari wanakuwa salama wanapokuwa kazini huku akisisitizia wamiliki wa habari nao kuwa makini na matamshi wanayotoa ili kutoweka rehani maisha ya waandishi.