Tuesday 16 September 2014

UCL: ENRIQUE KUMTEMA PIQUE BARCA KUIVAA APOEL JUMATANO?

  
PIQUE-BARCA-ATEMWABEKI wa Barcelona Gerard Pique amesisitiza hamna lolote kwa kuachwa kwake kuanza Mechi na Athletic Bilbao Jumamosi iliyopita huku Jumatano wakicheza Mechi yao ya kwanza ya Kundi F la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na APOEL Nicosia Uwanjani Nou Camp.
Kwenye Mechi hiyo ya La Liga ambayo Barcelona waliifunga Bilbao 2-0, Kocha Luis Enrique aliwapanga Masentahafu Javier Mascherano na Jeremy Mathieu na Pique kupigwa Benchi ingawa aliingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Mascherano.
Pique amekanusha kama ana bifu na Enrique na kudai ni uamuzi wa Kocha kubadili Kikosi chake.
Hata hivyo Pique amesisitiza yeye yuko fiti na yuko tayari kucheza wakati wowote Kocha akimchagua.
Lakini hadi Leo hamna fununu yeyote kama Kocha Enrique atampanga Pique kwenye Mechi hiyo ya UCL ambayo Barca wako Kundi F pamoja na hao APOEL, Ajax na Paris St-Germain.

0 comments: