Monday 29 September 2014

MWINJILISTI AUAWA NA MPENDWA WAKE AKIMFANYIA MAOMBI



KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, AHMED MSANGI.

MTU mmoja aliyehamamika kwa jina la AMBUMBULWISYE MWASOMOLA (35), ambaye ni muinjilisti na mkazi wa Kijiji cha Lukasi, ameuawa kwa kupigwa kichwani na mchi wa kutwangia.

Aliyefanya mauaji hayo amefahamika kwa jina la SWALAPO MWAISANILA (56), mkazi wa Kijiji cha Lwangwa ambaye ni mgonjwa wa akili. 
Tukio hilo lilitokea juzi TAREHE 27.09.2014 Majira ya SAA 23:30 USIKU, huko katika kijiji cha Luka, Kata ya Lwangwa, tarafa ya Busokelo, wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Mauaji hayo yalitokea baada ya Muinjilisti huyo wa kanisa la Baptisti kutaka kumfanyia maombi mtuhumiwa huyo kutokana na ugonjwa wa akili alio nao mtuhumiwa, ndipo mtuhumiwa alichukua mchi na kumpiga nao marehemu kichwani na kupelekea kifo chake.

MTUHUMIWA AMEKAMA
TWA.

0 comments: