Tuesday 30 September 2014

BAADA YA MATOKEO YA SIMBA KUA HABA PHIRI AHAMISHIA KAMBI DAR



Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema ulikuwa ni wakati mwafaka wa kuhamishia kambi jijini Dar.
Simba imehamishia kambi yake Changanyikeni jijini Dar na leo jioni imefanya mazoezini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Phiri amesema kwa muda waliokaa Zanzibar unatosha pia ni jambo jema kufanya mazoezi Dar es Salaam kwa kuwa wana mechi mbili ndani ya wiki mbili na zote zitapgwa Dar es Salaam.
"Mechi zote zitakuwa Dar es Salaam, wiki zote mbili tutacheza hapa. Hatuna sababu ya kurudi Zanzibar.
"Hivyo tutabaki hapa, naamini hata wakati wa mechi dhidi ya Yanga tunaweza kuendelea kubaki hapa," alisema Phiri.
Simba ilikuwa imeweka kambi mjini Zanzibar ambako ilikuwa ikisafiri kuja Dar es Salaam kila inapokuwa na mechi.
Chini ya Phiri, Simba imeanza mechi zake za ligi, zote kwa kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Coastak Union na baadaye 1-1 dhidi ya Polisi Moro.

0 comments: