Monday 29 September 2014

TIMU YA MBEYA CITY KUFUNGUA MADUKA YA JEZI,NA VIFAA VYA MICHEZO NDANI YA DAR


Mbeya City ina mpango wa kubadili jezi zake za awali kutokana na kutaka kuweka nembo ya mdhamini mpya Bin Slum na kuachana na zile za awali.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa usambazaji wa jezi mpya ambapo watasaka mawakala wa kuwasaidia kazi hiyo.

“Tupo katika mikakati ya kubadili jezi zetu ambapo zitauzwa katika maduka mawili jijini Dar, moja lipo maeneo ya Sinza na lingine litakuwa katikati ya mji, Posta.


“Tunawatafuta mawakala ambao watasimamia kazi hiyo kwa kuhakikisha tunadhibiti hali ya watu wengine kuuza jezi hizo na hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayehusika na utoaji wa jezi zetu bila ruhusa,” alisema Kimbe.

0 comments: