KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo amesema leo jioni ndiyo atajua kama kiungo wake, Andrey Coutinho anaweza kucheza au kutocheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam Maximo amesema hadi sasa, Mbrazil mwenzake huyo ana asilimia sawa za kucheza na kutocheza Jumapili ya leo. Kiungo huyo Mbrazil aliumia katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya juzi dhidi ya Polisi ya Dar es Salaam Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibio, Dar es Salaam. Andrey Coutinho anaweza kucheza au kutocheza Jumapili baada ya kuumia juzi
0 comments:
Post a Comment