Wednesday 17 September 2014

PIGO KWA ARSENAL, JACK WILSHERE AUMIA TENA ENKA YA MGUU

KOCHA Arsene Wenger amewalaumu wachezaji wake wa Arsenal kwa kushindwa kucheza vizuri wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund jana, huku akirejea na kiungo Jack Wilshere akiwa majeruhi baada ya kuumia kwenye mchezo huo.

Wilshere alitonesha enka yake ya mguu wa kulia kikosi cha Wenger kikilala 2-0 katika mchezo wa kwanza wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wlishere ameumia sehemu lie lie ambayo ilimfanya akawa nje ya Uwanja kwa miezi 17. "Ni vigumu kusema ni mbaya kiasi gani,"amesema kocha wa Arsenal. "Kwa kawaida haitakuwa mbaya sana, lakini nina wasiwasi mno kulingana na historia yake,".

Majanga; Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere akiwa chini baada ya kuumia jana
Wilshere has injured his right ankle, which has been problematic for him over the past two years
Wilshere ameumia sehemu lie lie ambayo imekuwa tatizo kwake kwa miaka miwli iliyopita

0 comments: