Sunday 28 September 2014

LEO SAMATTA KUIBEBA TP MAZEMBE KUIVAA AS VITA FAINALI?

 Klabu ya Congo DR, AS Vita, Jana imeifunga Klabu ya Tunisia Bao 2-1 katika Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Tunis, Tunisia na sasa wametinga Fainali kwa Jumla ya Bao 4-2 baada kushinda Mechi ya Kwanza pia 2-1.

MBWANA_SAMATTA_IN_TP
Hii ni mara ya kwanza kwa AS Vita kufika Fainali na watacheza ama na wenzao wa Congo DR TP Mazembe au Klabu ya Algeria ES Setif ambazo zinacheza Leo huko Lubumbashi.
TP Mazembe, ambayo kwao haifungiki na pia ina Mastraika mahiri kutoka Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wanahitaji kugeuza kipigo cha 2-1 cha Mechi ya kwanza ili kufika Fainali.
Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI itachezwa kwa Mechi mbil, Nyumbani na Ugenini, hapo Wikiendi yaOktoba 25 na Marudiano Novemba 1.
CAF CHAMPIONZ LIGI
NUSU FAINALI
RATIBA:
Marudiano
Jumamosi Septemba 27
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
20:00 Club Sportif Sfaxien 1 AS Vita Club 2 [2-4]
Jumapili Septemba 28
1600 TP Mazembe v ES Setif [1-2]

0 comments: