Kutoka kushoto ni Mwandishi wa habari wa ITV, Emmanuel Lengwa na mwandishi wa Chanel Ten, Rose Chapewa, wakichungulia kamera kuona ubora wa picha katika mji wa Mbalizi Mbeya, siku ya usafi uliofanyika juzi Juma mosi.
Katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akizoa taka kwenye ghuba la stendi ya umalila, Mbalizi Mbeya, juzi, alipoongoza suala la kufanya usafi katika mji huo kwa ushirikiano wa wakuu wa idara za Halmashauri hiyo na kikundi cha vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA), ambao wanafanya kazi ya usafi katika mji huo kwa kujitolea.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga,(kushoto), akimkabidhi Tsh.10,000/= mmoja wa watumishi wa halmashauri hiyo, baada ya juhudi zake za kufanya usafi siku ya jumamosi akishirikiana vema na kwa juhudi kubwa na vijana wa uviwamba na watumishi wenzake.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akihojiana na waandishi wa habari, ambao walifika eneo la usafi Mbalizi juzi. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akisukuma toroli lenye taka, akipeleka kwenye gari la taka tayari kwenda kumwagwa. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga,(kulia), akiwa na mratibu Mkuu wa kikundi cha UVIWAMBA, Gordon Kalulunga, wakifurahia jambo siku ya usafi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akihojiana na waandishi wa habari, ambao walifika eneo la usafi Mbalizi juzi. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, akisukuma toroli lenye taka, akipeleka kwenye gari la taka tayari kwenda kumwagwa. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga,(kulia), akiwa na mratibu Mkuu wa kikundi cha UVIWAMBA, Gordon Kalulunga, wakifurahia jambo siku ya usafi.
Na Angelica Sullusi, Mbeya.
WANANCHI wa mji wa Mbalizi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mkoani hapa wametakiwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kuhakikisha wanakuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka zinazozalishwa majumbani kwao ili kuhifadhi mazigira.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Upendo Sanga wakati wa zoezi maalumu la uondoaji wa taka katika baadhi ya maghuba yaliyopo katika mji wa Mbalizi lililowahusisha wafanyakazi hao pamoja na wananchi.
Sanga alisema kutokana na uzalishaji wa kata kuwa mkubwa unaosababishwa na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara katika eneo la Mbalizi kumefanya hata maghuba yaliyopo kuoneka hayatoshi..
“Hii ni changamoto kwetu kama Halmashauri na tutajitahidi kutenga bajeti kwa ajili ya huduma hii muhimu kwa jamii, lakini naomba wananchi hasa vijana pia watambue nafasi yao ya kujitolea kufanya usafi katika sehemu mbalimbali ndani ya halmashauri yetu hasa zenye uchafu mwingi uliorundikana,”alisema.
Kwa upande wake Mwanasheria wa halmashauri hiyo,Prosper Msivala alisema kwa sasa halmaashauri hiyo inaandaa sheria ndogo ambayo itawabana wananchi pindi wanapozalisha taka kuhakikisha wanazipeleka katika eneo lililohifadhiwa kuliko inavyofanywa sasa kuacha kata zikizagaa kila pahala.
Alisema kutoka na ukubwa wa halmashauri hiyo na miundombinu yake kuwa migumu suala la urundikanaji wa kata bado ni changamotio kwao kuzingatia kuwa wana gari moja na kuzolea kata tena zinazowekwa kwa mkono na trekta moja tu ambazo hazitoshi kumaliza tatizo, ikilinganishwa na kiasi cha kata kinachozalishwa kwa sasa.
Awali,Mratibu wa kikundi kinachojihusisha na masuala ya usafi kwa kujitolea mjini hapo kiitwacho Umoja wa Vijana Wazalendo mjini hapo (UVIWAMBA),Gordon Kalulunga alisema kikundi hicho kipo kwa ajili ya kuhamasisha vijana kutambua umuhimu wao kwa jamii.
“Sisi tuliamua kwa dhati kabisa kujitolea kufanya kazi hizi ili kuikumbusha jamii kuwa ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha inaweka mazingira katika hali ya usafi na si kuisubiri serikali tu,”alisema
Aidha,Kalulunga alisema kuwa nia yao ni kuhakikisha mwananchi anatambua kuwa kabla ya kudai haki yake kwa serikali basi hana budi kutimiza wajibu wake,huku akiwapongeza wafanyakazi wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao kuamua kuunga mkono juhudi za kikundi hicho kwa kushirikiana kufanya usafi pamoja.
0 comments:
Post a Comment