Monday 29 September 2014

KIBOKO AVAMIA KIJIJI WANANCHI WASHINDA JUU YA MITI KUTWA

 
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya Mashimboni  wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelazimika kushinda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko  aliyevamia kijiji hicho  na kuhatarisha uhai wa Wanachi 
 Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Mashimboni  Raphael  Kalinga  tukio hilo lilitokea hivi karibuni mwezi huu
 Akielezea tukio hilo alisema  Kiboko huyo baada  ya kuvamia kijiji hicho  alielekea kwenye nyumba ya mkazi  mmoja  aitwaye Joseph  Kashamakula  ambae alinusurika  kushambuliwa na Biboko huyo wakati alipokuwa  akitokea chooni kujisaidia 
  Diwani  Kalinga alisema  ndipo Kiboko huyo ambae  alionekana kuwa na hasira alipoanza  kukanyaga  kanyanga na vuvivunja vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa  nje ya nyumba yake na kuviharibu kabisa  hari ambayo ilimfanya wananchi huyo apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani 
 Majirani walifika kwenye eneo hilo  hata hivyo walilazimika  kutimua mbio  baada ya kiboko huyo  kuanza  kuwafuata  hari ambayo ilipelekea  kukimbia na kisha kupanda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na mnyama huyo ambae aliendelea kuvunja vyombo kwenye nyumba mbalimbali 
  Alisema  Kiboko huyo aliendelea kuzunguka kwenye eneo la kijiji hicho na  taarifa za  zilifika kwenye Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya  Nsimbo  ambao  walituma Akari wao wa wanyama pori kwenda huko 
 Baada ya  Askari wa Maliasli kufika kijijini hapo  walianza msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi  ambapo walifanikiwa kumwona na kisha  walimuuwa kwa kumpiga Risasi  tumboni na kichwani 
 Diwani   Kalinga  alieleza  baada ya Kiboko kuuwa  wananchi  licha ya hapo awali kumkimbia kiboko huyo  walianza  kugombea  nyama  ya  mnyama huyo  kwa kuchukua  kitoweo cha mboga na  baada ya nusu saa wakawa wamemmaliza 

Na  Walter  Mguluchuma 
 Mpanda Katavi 

0 comments: