KIUNGO wa Chelsea Cesc Fabregas ameweka historia katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka mchezaji wa kwanza kutoa pasi za mabao katika mechi sita mfululizo.
Huo ni mwendelezo wa tangu akiwa Arsenal, ambako alitoa pasi za mabao katika mechi zake mbili kubwa za mwisho kabla ya kuondoka The Gunners kurejea Barcelona mwaka 2011.
Fabregas amevunja rekodi kwa pasi mbili za mabao kwa Diego Costa kwenye ushindi wa The Blues wa 4-2 dhidi ya Swansea ambao unawaweka kileleni mwa Ligi Kuu England.
Fabregas akizozana na mchezaji mwenzake Diego Costa
Pia alimsetia Costa mabao aliyofunga dhidi ya Everton na Hazard dhidi ya Leicester akithibitisha kocha wa Chelsea Jose Mourinho hakukosea kumnunua.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alinza na moto wake katika urejeo wake England akiseti mabao ya Andre Schurrle na Branislav Ivanovic katika wiki ya kwanza ya msimu na Burnley.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, baada ya kung'ara Arsenal sasa anafanya vita pia Magharibi mwa London.
Fabregas alimsetia Robin van Persie kufunga wakifungwa na Bolton baada ya kutoka kumsetia Theo Walcott na van Persie katika sare ya 3-3 na wapinzani wao wa Kaskazini mwa London, Spurs.
Kabla ya mechi na Swans, Fabregas alikuwa miongoni mwa wachezaji sita waliotoa pasi za mabao katika mechi tano mfululizo walizocheza Ligi Kuu ya England.
Lakini shujaa huyo mpya wa Chelsea, sasa anawapiku Darren Anderton, Gianfranco Zola, Ryan Giggs, Thierry Henry na Antonio Valencia kwenye chati ya vinara wa kutoa pasi za mabao.
0 comments:
Post a Comment