KUFANYIKA DAR E S SALAAM SEPTEMBA 18-2014 UKUMBI WA MIKUTANO WA BENKI KUU YA TANZANIA BOT
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasaimezifungia kampuni 86 kufanyakazi ya ukandarasi baada ya kushindwa kufuata sheria za ujenzi. Hayo yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakatiakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu mkutano wa usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Septemba 18, 2014 jijini Dar es Salaam.
“Kazi yetu kubwa ni kusimamia sheria ya shughuli za ujenzi na kama tukibaini kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifungia kufanyakazi” alisema Jehad.
Alisema lengo mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta ya ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma hiyo.
Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa ambayo yanabomoka hapa nchini.Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti na ilivyosasa.
Dk.Mwakyusa alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepowataalamu wa majengo wanapotumia vifaa vya ujenzi
ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa hawana hatia.
“Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwaujumla kama ikiwepo sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya kutumiavifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiw zitumike aina gani kwenye jengo husika ,”alisema
Dk.Mwakyusa.Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo.
Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad akizungumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (katikati), akiwa na viongozi wenzake wa bodi hiyo. Kutoka kulia ni Kaimu Msajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala, Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad, Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Mwanasheria wa Bodi, Ibrahim Mohamed.
Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
0 comments:
Post a Comment