Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Stima Kabikile (katikati)
akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) wakati
alipofanya ziara yake ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Kinondoni
na Temeke kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na utendaji
kazi wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha
namna ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya (kulia) Ilala akimsomea
taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na mikakati yake ya kufikia
malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe. Waziri wa Fedha Bi. Saada
Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Temeke na
Kinondoni.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo
yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano
na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo
yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano
na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akiongozana na viongozi wa Manispaa
ya Kinondoni wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa
hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi
za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni
wananchi. katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Bw. Yusuph Mwenda
na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kulia) akisalimiana na
Waziri waFedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) mara alipowasili katika ofisi
za Manispaa hiyo kwa ziara ya kikazi katika jana kwaajili ya kupata
taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo zikiwemo njia wanazotumia kukusanya
kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni
wananchi.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akihutubia mkutano huku akisisitiza
juu ya kujikita zaidi katika kutumia TEHAMA katika kukusanya kodi za
majengo kama njia rahisi inayomrahisishia mlipaji kodi kuweza kulipa
kodi zake katika vituo vya huduma.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akipitia moja ya taarifa alizopewa na
uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni wakati alipofanya ziara yake
ya siku moja ofisi hapo.
……………………………………………………………………….
Na Rose Masaka.
WAZIRI
wa Fedha Bi. Saada Mkuya amefanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya za
Mkoa wa Dar es Salaam ili kupata taarifa za makusanyo ya kodi za
majengo ikiwa ni eneo moja kati ya maeneo sita ambayo yamepewa
kipaumbele katika suala la ukusanyaji wa kodi kama vile eneo la kilimo
na miundombinu.
Bi.
Saada Mkuya amesema kuwa aliahidi kufanya ziara hiyo katika kikao
kilichofanyika wiki iliyopita baada ya kurudisha zoezi la ukusanyaji wa
kodi za majengo katika Serikali za Mitaa ili kuona kinachoendelea,
kupata uhalisia na changamoto zinazowakabili watendaji wote wa Manispaa
ya Ilala, Kinondoni naTemeke.
“Tumerudisha makusanyo ya kodi za majengo kwenye mitaa kwasababu ni rahisi na wanajua nyumba zote” alisema Bi. Mkuya.
Kodi
ya majengo imekuwa ni moja ya chanzo kikubwa kinachotegemewa na
Halmashauri za wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam. Serikali iliona
hili mnamo mwaka 2013 na kuteua chanzo hiki kuwa mfano katika mpango
wake wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Kwa
upande wake Mweka hazina wa Wilaya ya Ilala Bw. Stima Kabikile amesema
kuwa Halmashauri ya Illala kupitia kitengo chake cha uthamini kwa
kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa wamejiwekea malengo ya
kuyatambua majengo 10,000 ambayo hayakuwepo katika jedwali la awali kwa
kutumia njia rahisi ya haraka ya uthamini.
“Tumeweza
kubaini na kuongeza idadi ya majengo 6,820 kati ya 10,000 tuliyokadiria
yenye thamani ya Shilingi bilioni 989.6 yenye tozo ya kiasi cha
shilingi trilioni 1.5 na kuweka kwenye mfumo tayari kwa malipo”. Alisema
Bw. kabikile.
Mtaalamu
wa kodi za majengo Wilaya ya Ilala Bw. Joseph Kawiche amesema kuwa kila
mmiliki wa nyumba hulipa kutokana na asilimia zake ingawa kuna baadhi
ya watu ambao hawajaona umuhimu wa suala hili na kuwa wanafichiana
majina,kwa hiyo wameona ni vizuri kutumia njia mbadala ya picha ili
kuwabaibni wanaokwepa kulipa kodi.
Kwa
upande wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Wilaya hiyo Bw.
Yusuph Mwenda amesema kuwa ameona umuhimu mkubwa wa kutumia Serikali za
Mitaa na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti ili
kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu kulipa kodi za majengo.
“Wenyeviti
wa mitaa 171,watendaji wa Kata 34 na Watendaji wa Mitaa 171 wanashiriki
na kuainisha majengo yaliyoachwa wakati wa uthamini”. Alisema Mwenda.
Mkurugenzi
wa wilaya ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa jumla ya
Shilingi bilioni 1.1 zimekwishakusanywa katika majengo 3123,aidha
majengo 3120 yaliyobakia yenye wigo wa kodi bilioni 1.4 yao katika hatua
nzuri ya ulipaji.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke amesema kuwa
Halmashauri imekusanya kiasi cha shilingi milioni 165.7 kutokana na
majengo ambayo awali hayakuwepo katika daftari la majengo ambapo mapato
yanatarajiwa kuongezeka kwa hali ya juu katika mwaka huu wa fedha baada
ya majengo yote 10,000 kuthaminiwa.
Baadhi
ya changamoto zinazozikabili Wilaya hizo ni pamoja na waraka wa msamaha
wa kulipa kodi ya majengo wakati sheria ipo kimya wakati wanamiliki
majengo ya makazi,kupangishana biashara ambao raia na wanajeshi
wastaafu wanao,pia shule binafsi kudai kutoa huduma wakati ada zao zipo
juu, hivyo Manispaa zote tatu zimetoa wito kwa wananchi wa Tanzania
kulipa kodi kwa hiari na Serikali iweke wazi sheria za misamaha kama
zipo.
0 comments:
Post a Comment