HOME »
» YANGA SC YAPANGWA KUNDI A PAMOJA NA WENYEJI RAYON SPORT KOMBE LA KAGAME
YANGA
SC imepangwa Kundi A katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Kagame pamoja na wenyeji, Rayon Sport, Coffee ya Ethiopia,
Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Katika
droo iliyopangwa leo mjini Kigali, Rwanda chini ya Katibu wa Baraza la
Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye,
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya
Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti. Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
 |
Yanga SC tayari wako katika maandalizi kwa ajili ya kombe la Kagame |
Droo ya michuano ya 40 ya CECAFA –Kagame ilihudhuriwa pia na viongozi wakuu wa Serikali ya Rwanda mjini Kigali leo.
Timu
14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo kuanzia Agosti 8 hadi 24 mwaka
huu- jumla ya mechi 34 zikichezwa katika viwanja vya Amahoro na
Nyamirambo, Kigali.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
Wizara
ya Michezo ya Rwanda na mashirika mengine yatadhamini michuano hiyo,
itakayokwenda sambamba na maazimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbau.
Televisheni
ya kulipia ya Supersport ya Afrika Kusini ambao ni maswahiba wa muda
mrefu wa CECAFA, ni miongoni mwa wadhamini pia na wataonyesha mechi zote
za michuano hiyo moja kwa moja. Ratiba ya mashindano hayo inatarajiwa
kutolewa wiki ijayo.
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment